KITABU CHA SOMO: Zaburi 9:1-2 ‘’Nitamshukuru BWANA
kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yake yote ya ajabu. Nitafurahi na
kukushangilia wewe; Nitaliimba jina lako wewe uliye juu
Na Bishop Burton Saulo Yuda wa
kanisa la Penueli Mpanda
Mtumishi wa MUNGU hapa anasema
atamshukuru MUNGU siku zote yaani siku zote za mwaka na haya ndiyo yanatakiwa
yafanywe na wewe ndugu yangu unayesoma ujumbe huu, na mimi naamini kila
mtu ana sababu ya kumshukuru MUNGU siku zote maana pumzi na uzima aliokupa
MUNGU ni zawadi ambayo lazima umshukuru MUNGU kila siku maadamu uko hai maana
ni kwa neema yake,
faida zake za kumshukuru
1.
Kwa wateule kumshukuru MUNGU ni
jambo la lazima maana kufanya hivyo inaonyesha kwamba ulimtegemea MUNGU
na ulihitaji msaada wake na bado unaamini hata kwa yale unayotarajia au
hujapokea, utapokea muda mfupi ujao.
2.
Kumshukuru MUNGU ni kurudisha
shukrani kwake kwa fadhili alizokutendea.
3.
Kumshukuru MUNGU ni kuthibitisha
kwamba MUNGU anaweza kukutendea muujiza hata kwa yale ambayo bado hujapokea
yaani kwa imani unaamini utapokea na kwa kweli tendo hili ni tendo la imani
sana yaani unakuwa na uhakika kwamba utapokea tu hata iweje.
4.
Kumshukuru MUNGU ni kumwonyesha
shetani na adui zako wote kwamba MUNGU ndiye msaada wako na atakushindia.
5.
Kumshukuru MUNGU ni kuonyesha kwamba
kiwango chako cha imani kwa YESU KRISTO ni kikubwa sana maana una uhakika
kwamba amekutendea tayari na bado atakutendea tena na tena. Ni tendo la imani
kwamba jambo hilo uliloomba kwa MUNGU tayari limetendeka kwenye ulimwengu wa
roho na sasa bado kidogo tu litatimia kwenye ulimwengu wa mwili.
6.
Kumshukuru MUNGU ni kuonyesha kwamba
shetani ameshindwa kwako.
7.
Kumshukuru MUNGU ni kumwaibisha
shetani na malaika zake.
Ndugu uwe katika imani na matendo
ambayo yanasema ‘’MUNGU ananionaje na sio kwamba watu wananionaje’’.
Ukimwangalia MUNGU utamshukuru kila
saa lakini ukiwaangalia wanadamu utashindwa kumpa MUNGU utukufu wake kwa
kumshukuru.
Ndugu yangu kushukuru MUNGU ni
jambo ambalo hata BWANA YESU alitufundisha mfano angalia
Mathayo 5:11-12..Heri ninyi watakaowashutumu
na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na
kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa ndivyo walivyowaudhi
manabii waliokuwa kabla yenu’’
Ndugu ni vizuri kusema ‘’Asante BABA
wa mbinguni’’ hata kama unapitia kwenye hali ngumu ila weka imani kwamba
MUNGU yuko pamoja na wewe na muujiza wako uko karibu sana.
BWANA YESU anatutaka tushukuru kwa
kushangalia na kufurahi.
1 Samweli 2:1,2,10,21.Naye
Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka
katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia
wokovu wako; Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote
ila wewe, Wala hakuna mwamba kama MUNGU wetu....... Washindanao na BWANA
watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu miisho
ya dunia......Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa
watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele
za BWANA.
Hana aliomba maombi ya shukrani
baada ya kupata mtoto Samweli na MUNGU baada ya maombi hayo ya kushukuru ya
Hana alimpa watoto wengine watano(5)
-Ndugu mshukuru MUNGU kwa hicho
kimoja alichokupa ili azione shukrani zako na kukupa vingine 5 kama alivyofanya
kwa Hana. Lakini kama tukiwa hatuna shukrani kwa MUNGU tunaweza hata
kunyang’anywa hata hicho kimoja tulichonacho.
Katika 2 Nyakati 20:21(Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele. )
ni mambo ya kumshukuru MUNGU pia katika
Zaburi 107:1(Mshukuruni
Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.), Zaburi 118:21 pia katika Isaya 12:4.
BWANA YESU alishukuru hata kabla ya kupokea kutoka kwa BABA yake iko Mathayo 26:27.
BWANA YESU alishukuru hata kabla ya kupokea kutoka kwa BABA yake iko Mathayo 26:27.
Katika Warumi 14:9 pia katika 1 Kor
15:57 Hii inaonyesha kumshukuru MUNGU ni jambo la lazima kwa wateule wake
KRISTO.
-Ndugu shukuru hata kwa ajili ya
wengine, shukuru kwa ajili ya mmeo/mkeo ambaye MUNGU amekupa, shukuru kwa ajili
ya Watoto wako ambao MUNGU amekupa, shukuru kwa ajili ya mchungaji wako, Mama
yako ,Baba yako, kiongozi wako na hata kazi yako ambayo MUNGU amekupa.
Waefeso 1:16 inatufundisha
kumshukuru sana MUNGU maana kwa kuonyesha shukrani ndio kuendelea kupokea
zaidi.
Tunatakiwa kumshukuru MUNGU bila
kukoma 1 Thesalonike 2:13 pia 1 Thesalonike 5:16:22. Na wakolosai 1:3.
Tudumu katika kuomba huku
tukimshukuru MUNGU kila iitwapo leo. Wakolosai 4:2.
MUNGU akupe ufahamu wa kumshukuru
siku zote katika jina la YESU KRISTO.
0 comments:
Post a Comment