PENUEL GLORIOUS MINISTRY OF TANZANIA

MAHUBIRI NA MASOMO YA KILA SIKU

PREACHER: SOMO :UTISHO WA KUFUFUKA Kitabu cha somo: YOSH. 5: 1 YOSH. 2: 1 – 24 Na Bishop ,Burton Saulo Yuda wa PGMT Mojawapo ya ahadi toka kwa Mungu wetu tunayemtumikia, ni pamoja na kutuma utisho wake mbele yetu (utisho wa Mungu wetu) huwa unatangulia daima mbele na kumfadhaisha adui yetu sana. Kutoka 23: 27 – 30 - Kwa kweli Yesu Kristo ni tishio, kwa wakuu wa dini ni tishio kwa Wafalme ni tishio, kwa mapepo na wachawi ni tishio, kwa wasomi ni tishio, kwa matajiri ni tishio, kwa askari ni tishio, kwa magonjwa na wafu ni tishio, nasi tunatakiwa kulijua hili na kulikiri daima hata tunapoona wengine wakiogopa na kukata tamaa kutokana na vitisho vya adui. Hes. 14: 6 – 9. - Mpaka leo duniani kote, kufufuka kwa Bwana Yesu ni tishio kwa imani nyingine zote ambazo waanzilishi wake na umaarufu wao hatimaye waliishia kaburini na hawakutoka kamwe hadi sasa ilibaki mifupa tu makaburini na nyama zao zikawa chakula cha mchwa!!. - Askari waliopewa kulilinda kaburi la Yesu, saa anafufuka walikipata cha moto!! Soma waliyoyakuta. Math. 28: 1 – 4, 11 – 15. - Habari hii ya kufufuka kwa Yesu imeenea dunia nzima na adui hata anapojaribu kuifunika kamwe hataweza, Yesu amefufuka na huu ndiyo ukweli, ndiye aliye na mamlaka juu ya kifo na siyo nabii au mtume mwingine yeyote, na kwa kweli huu ndiyo ushindi mkubwa sana wa Wakristo wa kweli. Ukitaka kujua kuwa Kristo ni tishio; soma (a) Marko 5: 1 – 15 (b) Yohana 11: 43 – 53 Kama ilivyokuwa katika nyakati za Joshua, ambapo watu wa Yeriko mioyo yao ilikuwa imeyeyuka na hofu ya Mungu kuiangukia Nchi ile; ndivyo ilivyo dunia hii ya sasa tunayoishi, pamoja na dini nyingi kujikakamua lakini viongozi wao wanajua kuwa Yesu Kristo ndiye nabii pekee aliye tishio, ambaye kaburi halikuweza kumshika, na habari zake zinaposhuhudiwa mahala popote kwa usahihi, zina uwezo wa kuwaondoa watu wa aina yoyote katika utumwa wao!!. Hakuna imani katika nabii yeyote leo hii hapa duniani iliyo na uwezo wa kumweka mtu huru zaidi ya imani ya Yesu Kristo. -Kama Joshua hakuna sababu ya kanisa kuishi kwa hofu hata kama dunia hii ingefanya vituko vyake ;bado tutaishi,tutakula,tutavaa,tutajenga,watoto wetu watasoma,watafanya kazi na biashara nzuri;Bwana amekwisha ondoa uvuli wanaojivunia. -Tunatamba kwa sababu mwanzilishi wa imani yetu hayumo kaburini ,amefufuka ,yu hai milele na milele ,anajipigania ,anasema,anatembea,anaishi,anazo funguo zote za mauti na za kuzimu,wana wa sayuni hatuna sababu ya kujikunyata. -Hakuna roho ya nguvu tena kwa shetani dhidi yetu,ona alivyo tishio huyu mwanaume.Luke.11:37-41. -Joshua alipata ushindi sana sababu ya ufahamu huu,adui zangu Mungu ametuma utisho kwao ,na mioyo yao tayari imeyeyuka na Bwana akusaidie neno hili kuwa

0 comments:

Post a Comment