KITABU CHA SOMO:1 Kor 6:17-18 '' Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,''
Maandiko hayo ni sehemu tu ndogo ya maandiko yanayolitambulisha Kanisa la KRISTO duniani.
Kanisa hai wametengwa na uovu wa dhambi na wametengwa na mambo ya kidunia yaliyo machukizo(Machafu).
Ndio maana huwezi kumuona Askofu akiwa disko akicheza.Huwezi kumuona Mkristo aliyeokoka akiwa kwa mganga wa kienyeji.Huwezi kumuona Mchungaji anatoa talaka.
Huwezi kumuona Mteule wa MUNGU akivuta sigara wala bangi na tena huwezi kumuona mteule wa KRISTO akitumia madawa ya kulevya.Huwezi kuona kanisa wakichukua mapanga na mikuki wakienda kulipiza kisasi kwa maadui zao.
Kanisa ndilo pekee linalosababisha amani Duniani.Kanisa ni la muhimu sana duniani.Siku Kanisa la MUNGU likiondolewa duniani ndipo neema itatoweka.
Kibiblia katika migao saba ya nyakati huu ni wakati wa Kanisa au wakati wa Neema.Kanisa la KRISTO ndilo pekee linalomwabudu MUNGU aliye hai na wa kweli.Kama kuna kanisa halijafikia hali hiyo basi hilo sio kanisa la KRISTO ila ni kanisa la kibinadamu tu.Katika Kanisa MUNGU ameweka viongozi na wasimamizi ili kazi ya MUNGU itendeke vizuri.
Matendo 20:28 '' Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi(Kanisa) lote nalo, ambalo ROHO MTAKATIFU amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.''
Kanisa ni la Muhimu sana ndio maana shetani huliwinda kanisa kuliko kitu chochote. Lakini kanisa linamshinda shetani kwa damu ya YESU KRISTO na kwa Neno la ushuhuda na kwa kuvumilia katika MUNGU aliye hai.
Ufunuo 12:11 ''Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.''
Kwa sababu kanisa ndicho kitu pekee ambacho shetani hakitaki basi amejribu mara kadhaa kuleta makanisa feki yanayomtukuza yeye na mengine yanamwabudu yeye, lakini hiyo haina maana kwamba kanisa la kweli halipo bali lipo na linazidi kuchanua.
shetani amejaribu kubuni dini nyingi sana lakini Kanisa la MUNGU lipo na litaendelea kuwepo na litaendelea kushinda na zaidi ya kushinda maana kanisa la KRISTO ndilo lililolibeba kusudi la MUNGU.
Madhehebu sio kanisa ila ni ni sehemu tu ambapo kanisa(Wakristo) wanakutana na kumwabudu MUNGU. Ndio maana wakati mwingine dhehebu moja linaweza kuhama kutoka kwa KRISTO kwa sababu ya viongozi wao waliojikinai lakini Kanisa la kweli la KRISTO bado lipo na linaendelea.
Hatuendi mbinguni kama dhehebu bali tutaenda mbinguni kama kanisa la KRISTO lililoshinda duniani.Kiongozi wa Kanisa akinaswa na shetani hakika kondoo kutawanywa kiroho itakuwa rahisi sana.
Mara nyingine tumesikia baadhi ya viongozi wa kanisa la kweli wakivamiwa na shetani na kuondoka katika kusudi la MUNGU.
Hapa nimekuandalia mambo saba ambayo mimi ninaona kama ndiyo yanayoweza kulitafuna kanisa la kweli.
1.Dhambi kwa viongozi wa kanisa.
Hosea 4:6 '' Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.''
Madhara makubwa zaidi yanayoweza kuliathiri kanisa ni dhambi kwa viongozi wa kanisa. Watu wa kanisani wanaweza wakaangamizwa sawasawa na watu wa mataifa kwa sababu ya viongozi wa kanisa. Kiongozi wa kanisa akiisahau sheria (Neno la MUNGU lote) anaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiroho kwa kanisa.
Kiongozi akiwa mdhambi itakuwa vigumu sana yeye kukemea dhambi katika kanisa na kwa njia hiyo watu wa MUNGU watakuwa wanaangamiza kwa kukosa maarifa.Kama mchungaji ni mzinzi ni vigumu sana yeye kukemea uzinzi.Kama Mchungaji ni mwizi ni vigumu sana kukemea wizi.
Kama Askofu ni muongo ni vigumu sana kukemea uongo kanisani.
2.Viongozi wa kanisa kutendea kazi kila neno wanaloambiwa na waumini au jirani wa waumini.
1 Timotheo 5:19-22 ''Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo. Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.''
Katika maandiko haya tunaweza kujifunza mambo mengi sana lakini kulingana na somo langu katika kipengele hiki cha pili, kunahitajika umakini sana kwa viongozi wa kanisa katika vile wanavyoambiwa na waumini au majirani wa baadhi ya waumini.
Kwanza kiongozi anapoambiwa jambo na mmoja wa waumini wake ambalo linamweka hatiani mtu mwingine haitakiwi kiongozi huyo kumwita haraka haraka tu mtuhumiwa na kumuonya au kumtenga, mambo hayo yanalitafuna sana kanisa leo.
Haina maana kwamba usifanyie kazi unayoambiwa na waumini wako au majirani wa waumini wako lakini hakikisha unafanya uchunguzi wa kina wewe mwenyewe ili pasitokee uonevu.
Kama kuna mtu umemuonea wewe mchungaji hakika mtu huyo hata kama atakuwa anakuja kanisani lakini hatakusikiliza na hatazingatia Neno la MUNGU unalomfundisha, hadi uweke mambo sawa.
Mara nyingine watu wenye makosa ndio huwa wa kwanza kukimbilia kwa Mchungaji ili kuwasema wengine kama njia ya kujisafisha na kuonekana wema.
Inawezekama mmoja wa wana kanisa anatuhumiwa na mtu mwingine wa kanisani kwamba ni mzinzi kwa sababu tu alionekana akitembea barabarani saa saba usiku.
Mchungaji kama atamwita mtuhumiwa haraka tu na kumfukuza kanisani au kumsema hadharani kanisani, na kama jambo hilo amesingiziwa hakika hapo kanisa litakuwa limetafunwa sana maana huyo naye anaweza akaanza kuitafuta haki yake kwa nguvu, anaweza akaacha kwenda kanisani na kujiangamiza kabisa, anaweza akarudi nyuma kiroho.
Kama amekosea inabidi kiongozi ajilidhishe kwanza ndipo atoe hukumu. Namna nzuri ya kujilidhisha ni kupata ushahidi kutoka kwa watu wawili au watatu ndivyo Biblia inashauri hapo juu.
Dhambi lazima zikemewe kanisani lakini iwe ni kweli dhambi imetendeka, sio kusingiziwa.Biblia inakushauri kiongozi wa kanisa kwamba usihukumu kwa haraka ila thibitisha kwanza. Usipendelee mtu, lakini kama utaamua haraka haraka tu mambo yanayowahusu waumini hakika unaweza kujikuta umependelea pasipo sababu.
3.Kuwepo wakala wa shetani katikati ya kanisa.
1 Yohana 4:1-3 ''Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua ROHO wa MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili yatokana na MUNGU. Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.''
Shetani hutaka sana kuingia kanisani ili aharibu utakatifu wa kanisa.
Kanisa ni lazima lisimame katika kweli ya Neno la MUNGU.
Viongozi wa kanisa ni lazima sana walisimamie kusudi la MUNGU kwa kulitii sana Neno la MUNGU.Kwa tamaa za pesa kuna baadhi ya watumishi hutunga vitu vya uongo ili tu kujipatia waumini au kupata pesa.
Sio kila miujiza ni ya MUNGU na sio kila anyehubiri watu ni anataka watu hao waende uzima wa milele. Kila mtu anaweza kuwa mchungaji akiamua lakini kama huyo hamtii KRISTO hakika huyo ni wakala wa shetani kanisani.roho ya mpinga Kristo ipo na kazi yake ni kuaondoa watu kwa KRISTO.
Hatuhitaji kumwabudu MUNGU kupitia sanamu au maji ya baraka, hatutakiwi kumwabudu MUNGU kupitia watu wanaojiita MUNGU.Tunatakiwa kumwabudu MUNGU kupitia YESU KRISTO na sio vinginevyo.
4. Kanisa kuacha maombi.
1 Thesalonike 5:17 '' ombeni bila kukoma; ''
Maombi ni maisha hivyo hayatakiwi kuwa ya msimu tu bali ya siku zote.
Kanisa likisahau maombi kuna madhara yatatokea maana kuona rohoni kutapungua, hamu ya kuendelea na wokovu itapungua.
Kanisa lisipokuwa na maombi ni rahisi shetani kupanda magugu ndani ya kanisa na kuyang'oa magugu hayo ikawa ni vigumu.Kanisa halitakuwa na maombi tu bali pia ni lazima kanisa liwe na maombi ya kufunga kila mara.
Kanisa kama mtu binafsi wa kanisani lazima afundishwa kuomba na kufunga na awe anafunga ili kunoa makali yake ya kiroho na ili aweze kujibiwa mahitaji yake anayoyataka.Kuna mengine hayawezi kuondoka katika kanisa hadi kanisa lifunge na kuomba.
Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''
5. Kanisa kutembea katika maono ya uongo yanayoambatana na ujanja ujanja wa watumishi.
Mathayo 15:8-9 ''Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.''
Kama kanisa litamwacha KRISTO na Neno lake hakika shetani atachukua nafasi tu na jambo hilo kupelekea uongo kuanza kuliendesha kanisa.
shetani akitawala kanisa ni lazima waumini wawekewe mipaka na kufundishwa kujiona kwamba wao tu ndio kanisa na kwingine kote ni kwa shetani.
Biblia ndio inatakiwa iwe ushahidi na sio watumishi kuwadanganya watu.
Sio kila mchungaji au Askofu ameitwa na MUNGU, Wengine wamejita na wengine wameitwa na shetani.
Shetani ni baba wa uongo hivyo na watumishi wake lazima wabuni vitu vya uongo na lazima kanisa litembee katika maono ya uongo, mambo haya yanalitafuna kanisa sana.
Leo kuna wachungaji hawamhubiri KRISTO tena bali wanajihubiri wenyewe na kudanganya watu.
Kanuni ya Biblia pia inatafasiriwa vibaya na baadhi ya watu. Ngoja nikuambie; Japokuwa Ibrahimu Ni Baba Wa Imani Lakini Hiyo Haina Maana Kwamba Sara Ni Mama Wa Imani.
Mambo Ya Kiroho Huwa Tofauti Na Mambo Ya Kibinadamu. Tukiruhusu Kanisa Liifuate Dunia Basi Ipo Siku Tutasikia Kwamba Stephano Au Ayubu Ni Babu Wa Imani.
Dunia Leo Imeingia Kanisani Ndio Maana Kuna Mawakala Wa shetani Hujipachika Katika Baadhi Ya Maandiko Na Kudai Maandiko Hayo Yaliwatabiri Wao. Kuna Watu Hudai Wao Ni Eliya Amerudi Duniani, Kuna Watu Hujiita Kristo, Kuna Watu Hujiita Henoko Aliyerudi Duniani, Wengine Hudhani Kuna Mtu Anaitwa Mama Wa Mungu leo.
Kuna Watu Hujiita Mungu Muumbaji Aliyekuja Kuishi Na Wanadamu Na Kuna Waongo Original Hudai Biblia Iliondolewa Zamani Na Kuja Kitabu Kingine.
Kanuni Ya Biblia Iko Tofauti Sana Na Kanuni Za Kibinadamu Au Kanuni Za Kimwili.
Ukitaka Biblia Ikufuate Utaishia Pabaya. Wewe Mwanadamu Ndio Unatakiwa Uifuate Biblia. Biblia Haiwezi Kubadilishwa Na Mazingira Wala Haiwezi Kubadilishwa Na Wanadamu. Kataa Kuokoka Harafu Utarajie Mbingu, hakika hakuna mbingu kwa wanaokataa kuokolewa na BWANA YESU
(Yohana 3:16-21). Mkatae YESU Ukidhani Utafika Mbinguni, hakika huwezi kufika(Matendo 4:12)
6. Kanisa kukosa upendo.
1 Petro 1:22-23 ''Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. ''
Upendo wa KiMUNGU ni hali ya kumpenda mtu bila kujali mtu huyo alivyo au ana sifa gani.Lazima kanisa liwe na upendo. Kanisa lazima limpende
mchungaji wao na sio kumsema vibaya.
Kumbuka kuwa mkimsema vibaya mchungaji wenu hakuna atakayemsema vizuri huko nje, hakuna atakayekuja kuokoka maana atadhani kanisa halifai kumbe ni kukosekana kwa upendo.
Lazima kanisa wapendane wote bila kujali cheo cha mtu au hadhi ya mtu. Ukikosekana upendo wa KIMUNGU kanisani hakika jambo hilo litalitafuna sana kanisa na kanisa halitastawi kamwe.
1 Kor 13:4-7 ..''Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.-
7. Kutokubali kukosolewa au kusahihishwa.
1 Kor 8:2 ''Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.''
Hakuna mwanadamu anayejua yote na hakuna mwanadamu anayeweza yote.Katika kanisa wote tunategemeana.
Hata Mchungaji kuna baadhi ya mambo hajui na anahitaji kusaidiwa, Hata mama mchungaji sio kwamba anajua yote kuliko wanawake wote kanisani.
Sio kwamba wazee wa kanisa hawana la kusaidiwa bali yapo tena mengi.
Sio kwamba matumizi ya kanisa yakienda vibaya basi wanaotaka kushauri wafukuzwe kanisani.
Vitu vya kanisa ni vya kanisa na sio mali ya kiongozi wa kanisa hivyo kuna wengine akitaka kusaidiwa tu kwa upole anaanza kuhubiri kwamba roho ya uasi na kukosa heshima imeingia kanisani.
Kama Mchungaji angekuwa anajua yote ana anaweza yote basi kusingekuwepo kiongozi wa ibada kanisani, kusingekuwepo mashemasi kanisani, kusingekuwepo wapiga vyombo na kusingekuwepo waimbaji. Lakini kwa sababu kila mtu kanisani ni muhimu basi ni muhimu sana kusaidiana ili kuondoa lawama zisizokuwa na sababu.
MUNGU AKUBARIKI SANA
Tuesday, July 6, 2021
HATUA ZA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI
Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’ (1Timotheo 4:12 & 14).
Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo.
Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingereza la ESV unasema ‘Keep a close watch on yourself and on the teaching. Persist in this, for by so doing you will save both yourself and your hearers’. Kwa mujibu wa dictionary ya kigiriki na kiebrania neno ‘save’ lina maana ya kuweka huru (deliver), kulinda (protect), kuponya (heal), kutunza (preserve), kuokoa (save). Jambo muhimu ambalo Mtume Paulo alikuwa akilisisitiza hapa ni hili; jambo muhimu si tu kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako, bali kila mwamini ana kazi kubwa ya kufanya ili KUULINDA NA KUUTUNZA WOKOVU WAKE.
Moja ya changamoto kubwa sana ambazo zinawakabili vijana wengi waliokoka leo ni kuipenda dunia. Kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana wengi na kwa sababu ya kuipenda dunia; (a) Mahusiano ya vijana wengi na Mungu wao yameharibika (b) Maisha ya vijana wengi yamekosa uelekeo (c) Kutokana na uovu wao jina la Bwana Yesu limekuwa likitukanwa.
Katika kile kitabu cha 1Yohana 2:16 ni dhahiri kwamba dunia imejaa TAMAA YA MWILI, TAMAA YA MACHO NA KISHA KIBURI CHA UZIMA. Tamaa ina nguvu ya kuvuta pamoja na kudanganya, naam inamuingiza mtu kwenye jaribu. Hii ina maana tamaa ni mlango, naam mlango huu unapaswa kufungwa mapema usikupoteze. Hebu tujifunze kutokana na anguko la mfalme Daudi na mke wa Bathssheba (Samweli 11:1-2). Tunaona anguko la Daudi lilisaabishwa na kumpa Ibilisi nafasi kwa kutokwenda vitani. Mkristo akipoa katika kuvipiga vita vya kiroho inakuwa rahisi kwake kuanguka dhambini (Yakobo 1:14-15), naam kumbuka kwamba siku zote tamaa inalenga kumfurahisha mtu binafsi (self-pleasing) bila kujali matokeo yake.
Hivyo katika nyakati tulizonazo sasa suala la kuipenda dunia ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa vijana wetu. Ujumbe huu mfupi unalenga kueleza kwa namna gani kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana na nini vijana wafanye ili kuikabili na kuishinda changamoto husika.
Pia katika waraka 2Timotheo 2:15 Mtume Paulo anaendelea kumwambia kijana Timotheo ‘Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli’.
Pengine kila mmoja wetu atafakari maisha yake kwa kuhusianisha na maelekezo ya Paulo kwa Timotheo. Naomba jiulize na kujijibu kwa uaminifu kwamba mosi, je, ujana wako wako unaheshimika au unadharauliwa? Pili, je, kwa waamini wenzako umekuwa kielelezo cha kweli kwa habari ya imani, upendo, usafi, usemi na mwenendo au la?
Binafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwa namna gani kijana atahakikisha kwamba (a) Ujana wake haudharauliwi (b) Anakuwa kielelezo kwa waamini wenzake (c) Anathibitisha kwamba kweli amekubaliwa na Mungu. Naam katika kusoma na kutafakari neno la Mungu nimejifunza kwamba zifuatazo ni njia ambazo zitatusaidia sisi vijana wa leo kuifikia kweli hii ya neno la Mungu.
• Kijana adumu katika kuomba na kusoma (kutafakari + kulitenda) neno la Mungu
Katika Zaburi 119:9 & 11 Biblia inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii AKILIFUATA neno lako’. Pia kwenye ule mstari wa 11 inasema ‘moyoni mwangu nimeliweka neno lako, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI’.
Naam katika Mathayo 26:41 imeandikwa ‘Kesheni, mwombe, MSIJE mkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu’. Yohana 17:17 inasema ‘uwatakase kwa ile kweli ;neno lako ndiyo kweli. Mambo haya mawili yanapaswa kwenda kwa pamoja nakijana akidumu katika kuomba na kusoma neno la Mungu ushindi ni lazima.
• Kijana asimpe Ibilisi nafasi.
Kijana anapaswa kujiuepusha na mazingira yenye kumfanya aiepende na kuifuatisha namna ya dunia hii. Katika kitabu cha 1Wakorinto 6:12 imeandikwa ‘Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote VIFAAVYO; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya UWEZO wa kitu chochote’. Ni vizuri ukahakikisha kwamba ufahamu wako hautawaliwi na mambo yasiyo ya msingi (non-essentials of life) – Je ufahamu wako umetawaliwa ni nini?
Hii ndiyo sababu iliyomfanya Paulo awaambie Waefeso ‘Wala msimpe Ibilisi nafasi’ (Waefeso 4:27) na pia awaambie Warumi “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake’. Toleo la KJV linasema ‘But put ye on the Lord Jesus Christ, and MAKE NOT PROVISION for the flesh, to fulfill the lusts thereof’. Na toleo la ESV linasema ‘But put on the Lord Jesus Christ, AND MAKE NO PROVISION FOR THE FLESH, TO GRATIFY ITS DESIRES’ (Warumi 13:14). Je hivi leo ni kwa namna gani vijana wanaungalia mwili na kumpa Ibilisi nafasi? – Mitandao ya kijamii, kuangalia na kusoma vitu vichafu, hasira, mawazo, mazingira.
• Kijana azikimbie tamaa za ujanani
Katika 2Timotheo 2:22 imeandikwa ‘LAKINI ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi’. Kijana anawezaje kuzikimbia tama za ujanani? Hebu tuangalie mfano wa Yusufu. Ushindi wa Yusufu dhidi ya mke wa Uria (Mwanzo 39:2-9). Hii ni habari ya kijana Yusufu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mali za Potifa.
Pamoja na ushawishi aliokutana nao Yusufu alijibu kwamba ‘Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?’ Mwanzo 39:12 inasema ‘huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake akakimbia akatoka nje. Ili kuzikimbia tamaa za ujanani kijana anapswa (a) ajiepushe na mazingira/marafiki wabaya (Mithali 1:10 & 1Wakorinto 15:33) (b) Ajitenge na uovu (Mithali 16:17, Zaburi 1:1).
Ni muhimu ukakumbuka kwamba hukupewa mwili kwa ajili ya zinaa maana miili yenu ni ni viungo vya Kristo na tena hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 6:15 & 19), tena yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorinto 6:17) maana tena imeandikwa ‘Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili’ (1Wakorinto 6:13b). Tena imeandikwa ‘Lakini uasherati USITAJWE kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu’ (Waefeso 5:3).
• Kijana ajifunze kuenenda kwa roho na si kwa mwili
Katika wagalatia 5:16 imeandikwa ‘Basi nasema ENENDENI KWA ROHO, wala HAMTATIMIZA kamwe TAMAA ZA MWILI. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayoyataka’.
Je kuenenda kwa Roho ndio kukoje?
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote (Yohana 16:13) na pia imeandikwa ‘kwa kuwa wote WANAOONGOZWA na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’ (Warumi 8:14). Kuenenda kwa Roho ina maana ya kuishi kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako (Warumi 8:2).
Naam kadri unavyokuwa mtiifu kufuata utaratibu wake ndivyo unavyokuwa mbali na sheria ya dhambi na mauti ambayo ni mwili. Kumbuka imeandikwa ‘kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waiufuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani (Warumi 8:5-6) na pia Wafilipi 4:8.
Naam imeandikwa ‘Kila mmoja wenu ajue KUUWEZA MWILI wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu HAKUTUITIA UCHAFU, bali tuwe katika utakaso’ (1Thesalonike 4:4-5, 7). Ni jambo la ajabu sana kwamba kwamba tumepewa fursa ya kuiweza miili yetu. Ndio tunapaswa kuuweza mwili kwa maana ya kuudhibiti kwa kuuongoza na kuufanya ufuate nia ya roho.
Kijana mwenzangu kama umechagua kumpa Yesu maisha yako kwa njia ya wokovu, nakusihi na kukushauri zingatia haya ili kuwa na maisha yenye kielelezo na ushuhuda mzuri maana imeandikwa ‘Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa’ (2Petro 2:20-21).
AMENI
Wednesday, June 30, 2021
SOMO: SUMU YA SHETANI KWENYE MOYO -2
2. Anabadilika badilika kwenye maamuzi yake
Mtu ambaye ana sumu ya shetani moyo wake unatema mauti badala ya uzima. Wakati Wayahudi wanatafuta namna ya kumuua Yesu,
ndipo shetani akamwingia Yuda na kisha akasema na wakuu wa makuhani akasema nao jinsi ya kumtia mikononi.
Kwa hali ya kawaida mtu hawezi kumuuza baba yake, lakini baada ya kutiwa sumu Yuda alibadilika maamuzi yake na akaenda kujadiliana na wakuu na makuhani namna ya kumtia Yesu hatiani.
Luka 22:3-4.. “Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.”
Unakuta mtu anawazo zuri sana juu ya maisha yako na anakwambia nitakupa mtaji, nitakupa biashara lakini Shetani akimwingia anabadilika kabisa.
Yuda alikuwa ni mtu mzuri kabisa anatunza fedha za huduma ya Yesu, lakini Shetani alipomuingia andipo akaanza kufanya maamuzi ya kumuuza Yesu.
Yohana 13:2.. “Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti;”
Sio kwamba shetani aliweka moyo mwingine ndani ya Yuda bali aliweka sumu kwenye moyo wa Yuda.
Aliweka kitu cha usaliti, yaani uasi, ukawekwa kwenye moyo wa Yuda ndipo sasa akaanza kuwaza kumsaliti.
Sumu ndio hiyo mipango ya usaliti. Ukiona mtu alikuwa na bidii kanisani tena amefika kuitwa Pastor, lakini gafla akaacha hata hasalimii njiani ujue Shetani ameweka sumu ndani ya moyo wake.
Sumu ya Shetani inaharibu tabia za watu, unashangaa watu wawili wanafunga ndoa kanisani na walipooana waakaitana majina yote ya kimapenzi lakini gafla unashangaa mmoja anasema simpendi huyu, simtaki huyu. Ni kwamba Shetani ameweka sumu ndani yake, ikambadilisha moyo na mawazo yake.
Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. Akamshawishi kwa maneno mengi lakini bada ya kulala naye akamchukia sana.
Unajifunza kwamba unaweza kudanganywa kwa maneno matamu na kaka yule lakini baada ya kubali kulala naye anakuchukia machukio makuu. Wewe binti, usikubali kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa, hata kama unadanganywa kwamba atakuoa usifanye hivyo.
2 Samweli 13:14-15 “Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.”
Linda sana moyo wako kuliko vyote ulivyonavyo, ukiona kijana unafanya tendo la ndoa kabla ya ndoa na anasali kabisa kanisani ujue moyo wake tayari umeharibika.
Miaka ya nyuma mkristo kupata mimba kanisani lilikuwa ni jambo la aibu na kuogopa lakini siku hizi jambo hili limekuwa ni kawaida kabisa.
Bibilia inasema ikimbieni zinaa (1Wakorintho 6:18) lakini utashangaa mtu unashikwa mkono unapelekwa hadi gest, unapelekwa hadi porini lakini bado unasema Shetani mekupitia. Na kwa sababu hiyo utaomba sana, utaimba sana kama huachi hayo huwezi kufanikiwa.
Kuna wakati unaomba lakini macho ya Mungu hayakuoni, wala sikio lake halikusikilizi maombi yako. Ni kwa ajili dhambi zako zinafanya Mungu asikii maombi yako; unaweza kuwa wengi sana na Mungu akasikia kwa mtu mmoja na mwingine asisikie. Ni kwaajili ya moyo uliojaa sumu; Shetani anakujaza uongo hatimaye unafanya makosa na unasema Mungu ni mwenye rehema. Hakika huwezi kufanikiwa.
2 Nyakati 7:14-17 “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu;”
3. Mauti
Ndani ya moyo zikiingia sumu uhai unaondoka. Shetani akijaza sumu vile vitu vinavyoleta uhai ndani yako vinakufa na sumu inajaa ndani yako inakuathiri wewe na watu.
Sumu hii itakufanya kudanganyika na ukidanganyika moyoni na kufanya maamuzi yasiyo sawa hatima yake ni lazima utakufa. Sumu ikiingia ndani yako hata kama upo salama leo siku moja utakufa mambo yako yatakufa, kazi yako itakufa kila kitu chako kitakufa.
Matendo 5:5-11.. “Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya…. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.”
4. Anafanya vitu ambavyo sio hiari yake
Kuna vitu unafanya sio kwa hiari yako, Shetani anasababisha ufanye si kwa nguvu zako. Shetani akiingia ndani ya moyo anakulazimisha.
Kuna mambo unafanya ingawa ni mabaya lakini unayafanya kwa sababu Shetani ametia sumu kwenye moyo wako na hutendi kama wewe na kwa maamuzi yako, si kwahiari yako.
Warumi 8:19-20 “Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha katika tumaini”
Ukisikia habari za yule mtu ambaye alikuwa anakaa makaburini, ameacha nyumba yake na ndugu zake na kisha kuamua kuishi makaburini. Alikuwa anakimbizwa hadi jangwani kwa nguvu za pepo. Ndipo sasa unaona mtu anakimbia mume, anakimbia mke, anakimbia biashara kwa nguvu za pepo.
Luka 8:29.. “Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo.”
Watu wengi wamefeli masomo, wameshindwa kazi, wameacha ndoa ukimuuliza anasema nimesikia moyo wangu unasema, nimesikia roho mtakatifu anasema na mimi. Huyo sio roho mtakatifu ni roho mtakafujo. Roho mtakatifu hawezi kukutenga na watu, hawezi kuvunja ndoa yako.
Unahitaji moyo wako uwe salama siku zote kwa maana moyo ukijaa sumu fikra zako zina haribika. Ndipo unaona mtu alikuwa anamsifia sana mume wake lakini gafla sasa anamchukia sana kuliko chochote, hawezi kuizuia wala kuitawala nafsi yake.
Hawezi kuizuia nafsi yake, unamwambia mtu kabisa tabia hii ni mbaya uiache lakini hawezi kuacha kwa sababu hawezi kujizuia; moyo wake umejazwa sumu.
1Timotheo 5:6.. “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.”
Ukiona umekuwa mgumu sana na utoaji kanisani ujue moyo wako umejazwa sumu, ni sawa na vile Anania na mke walipatana kumdanganya Roho Mtakatifu.
Sio wewe ufanyae bali sheria ya dhambi ikaayo ndani yako, yale mambo unayapenda huwezi kuyafanya lakini yale ambayo hutaki kuyatenda ndio unayatenda. Ndani ya moyo wako umejazwa na mambo ya mabaya; ndio maana unawaza na kutenda mabaya. Leo Bwana akuponye kwa jina la Yesu.
Moyo ukipata madhara, yale unayoatenda si wewe bali ile sumu ikaayo ndani ya moyo wako; kuna maamuzi umefanya ambayo sio sawa, ni ya maamuzi yaliyoathirika na sumu ya Shetani.
Moyo wako ukihuishwa na uahi ukabaki ndani yako utafanya yale mazuri, hakuna atayakulazimisha kwenda kanisani, hakuna atakayekulazimisha kutoa kwajili ya Bwana utajikuta unafanya mwenye kwa kupenda.
SOMO: SUMU YA SHETANI KWENYE MOYO WA MWANADAMU -1
KITABU CHA SOMO. Matendo 5:3-4.."Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.”
Na Askofu Burton Saulo Yuda wa Kanisa la Penuel Mpanda
Utangulizi
Wakati unataka kujifunza somo hili kuna vitu unapaswa kujiuliza; kwamba ni kweli Shetani anaweza kuujaza sumu moyo wa mtu ? na Je anaweza kuujaza sumu moyo wako wewe? Je ni kweli Shetani anazo sumu za kumjaza mtu? Je Shetani anaujaza moyo mambo gani ambayo ni sumu? Je, vitu hivyo vinavyoitwa sumu vinafaida au hasara? Mwisho wa somo hili moyo uliojaa sumu ili ufe Bwana anaenda kuuganga tena kwa jina la Yesu.
MOYO KUJAZWA SUMU NA SHETANI
Kabla sijakuelezea ni namna gani Shetani hujaza sumu na kwa njia gani, ngoja nikueleze kidogo kuwa Shetani ni nani.
Shetani kwa asili anajulikana kama ni mwizi; huyu anayejaza watu sumu anafanya kazi kuu tatu kwenye maisha ya watu, kwanza ni mwizi. Wakati wowote aonekanapo huja kwa lengo lake la kuiba. Kazi yake ya pili ni kuua yaani aonekanapo popote huja kwa lengo la kuondoa uhai kwenye maisha ya watu na kazi yake ya tatu ni kuharibu, yaani akija kwenye maisha ya mtu huja kwa lengo la kuharibu kila kitu alichonacho. Imeandikwa;
Yohana 10:10.. “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
Mahali pengine Shetani anaitwa Mharabu. Sio muharabu yule wa Dubai unayemjua kuwa ni mweupe kwa sura, hapana. Mharabu huyu kwa kiingereza anaitwa Destroyer au mwenye uwezo wa kuharibu. Kwa Kiswahili cha kwaida angeitwa muharibu lakini kwa kiswahili fasaha anaitwa Mharabu na lengo lake ni kuharibu kila kitu masomo kazi, ndoa, biashara n.k.
1 Wakorintho 10:10… “Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.”
Mahali pengine Shetani anajulikana kama muongo na na baba wa uongo. Shetani ni mshawishi wa mambo maovu anashawishi watu hadi wanaharibikiwa. Aliwahi kumshawishi mfalme Daudi kuwahesabu wana wa Israeli kinyume na mapenzi ya Mungu akasababisha Daudi kumkosea Mungu. Shetani akikushawishi unathiriwa moyo na hatimaye unaanza kutenda mambo ambayo si sawa.
Shetani mahali pengine anajulikana kama mpanzi wa mambo mabaya kwenye Maisha ya watu. Anaweza kutia vitu vibaya kwa mtu na likakua kama pando baya na hatimaye maisha ya mtu yakaharibika kabisa. Ndio maana Bwana Yesu akasema kila pando lisilopandwa na Baba wa mbinguni litang’olewa kwa sababu Shetani naye hupanda mabaya kwa watu. Shetani anaweza kumtia mtu kifafa, anaweza kutia mtu ujinga, magonjwa n.k.
Mathayo 15:13.. “Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.”
Kwa sababu hiyo Shetani anaweza kuingia kwenye maisha ya mtu kwa makusudi mengi kama nilivyokueleza. Anaweza akaja kama mtu na kusema nawe na kisha kukupandia au kukutia sumu.
Shetani anaweza kuongea na mtu na akisha sema naye roho ikamuingia. Kama aliweza kufika kwenye kiti cha enzi cha Mungu na akaanza kusema na Mungu
(Ayubu 1:6-7) anaweza pia kumsemesha mtu sumu ikamuingia na mipango ya maisha yake ikaaanza kuharibika. Kwaajili ya kusemeshwa na Shetani ndipo utaona mtu alikuwa na juhudi kwaajili ya mambo ya Mungu gafla anaacha. Neno moja alilolisikia kwa Shetani likaharibu moyo wake na akaanza kuacha mambo yake ya msingi, akaanza kufanya maamuzi mabaya hatimaye anaharibikiwa.
Shetani anaweza akaja kama Rafiki lakini kumbe ni yeye katika umbo la kibinadamu ili usijue. Mahali unapoishi mambo yako yameanza kuharibika, upendeleo wako kati yako na Mungu, na watu umepungua sana kwa sababu ya ile sumu iliyokuingia. Yule aliyekusemesha ukabadilika moyo wako ukaacha kumtumikia Mungu, ukaacha huduma, ukamuacha mke wako/ ukamuacha mume wako huyo aliyekusemesha sio mtu hata kama unakaa naye chumba kimoja ni Shetani kwenye mwili wa mtu.
Kama vile Mungu akikusemesha roho inakuingia na kukusimamisha vile vile Shetani akikusemesha roho inakuingia na kukuangusha. Unaweza kusemeshwa ukaharibikiwa na kukosa imani juu ya Mungu na ukafanya mambo ya ajabu.
Yale maamuzi uliyofanya ukamuacha mke wako/mume wako siku hizi uko single unahaha ni kwaajili ya moyo wako kujazwa sumu. Miaka yote mlikuwa pamoja mkipendana na kuitana kila aina ya majina ya mapenzi imekuwaje leo unampiga, unamtukana? Ni kwa ajili ya sumu ya Shetani. Unakuta mtu ni mlokole kabisa lakini anakuja kwa mwenzake anamwambia uache kusali, unajiuliza ni mtu huyu kweli? Sio mtu ni shetani katika umbo la binadamu.
JINSI YA MOYO UNAVYOTIWA SUMU
Moyo ni kituo kikuu (centre) cha maisha ya mtu ya kiroho na kimwili. Moyo ndio unabeba mambo yako yote ya kimwili na kiroho. Moyo ndio unawakilisha uhai wa asili wa mtu au ni chemichemi ya uhai wa mtu. Ndani ya moyo ndiko unapata uhai. Ndio maana bibilia ianasema linda sana moyo wako kuliko chochote. Sehemu nyingine moyo unawakilisha uamuzi wako au fikra zako hivyo ni kitu cha msingi kuliko vyote.
Mithali 4:23… “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”
Mungu anaagiza kwamba moyo wako unapaswa kulindwa kuliko kitu chochote. Kama kungelikuwa na uwezo wa kutumia silaha, basi unapaswa kuchukua bunduki kubwa na kuulinda moyo wako. Anasema linda sana moyo wako kuliko mke wako, kuliko mume wako, kuliko fedha au gari lako. Jiulize mbona wanajeshi hulinda mipaka ya nchi na raia wote, kwanini wewe hulindi moyo wako? Nakukumbusha leo kwa jina la Yesu unapaswa kulinda moyo wako kuliko yote uyalindayo.
Shetani akishatia sumu kwa watu, unashangaa mtu anamwambia girl friend wake au boy friend ninakukabidhi moyo wangu? Jinsi gani asivyothamini moyo wake na hatimaye anapata matatizo makubwa. Unamsikia mtu anamwambia mwenzake kaa hapa nikueleze siri zote za moyo wangu, huyu athamini moyo wake kabisa. Bibilia inamtaja Samson kwa kosa lake kueleza siri zote za moyo wake na matokeo yake alitobolewa macho na kuteswa.
Unajifunza usipolinda moyo wako kwa kusema kila kitu kilichomo ndani yako utatobolewa macho. Unashangaa magari yanalindwa, mashamba yanalindwa kwa alarm za bei kubwa kwa nini sasa moyo wako hauna ulinzi. Unatakiwa kuweka makombora kulinda moyo wako. Moyo usiokuwa na ulinzi utajazwa sumu na Shetani. Na Shetani akijaza sumu moyo wako hakika utaaribu ndoa yako, utaaribu kazi yako, utaaribu maisha yako na kila kitu chako kitaharibika .
Moyo usipolindwa kuna chemchem za sumu zinaanza kuingia ndani yake. Sumu hizi huingia kwa njia nyingi hasa kwa kupitia maneno. Kuna mtu akikusemesha hakika mdomoni mwake inatoka sumu na ikikuingia moyo wako wote unaharibika. Unaweza kuambiwa jambo na mtu gafla ukaanza kumchukia mtu na tabia yako ikaharibika ukawa mtu wa tofauti kabisa, hivyo linda sana moyo kuliko vyote uvilindavyo.
Shetani haangaiki sana na pua yako wala miguu, anahangaika na moyo ili pale uzima unapotoka patoke mauti. Unaweza ukawa umeokoka, ukaacha moyo wako bila ulinzi hakika utaharibikiwa. Mtu akisema na wewe angalia sana maneno yake maana yanaweza kuwa sumu kwako. Kuna vitu unafanya kwa hasira, uchungu kwa sababu kuna vitu vimekaa kwenye moyo wako kama sumu, leo Bwana akuponye kwa jina la Yesu.
Baada ya Shetani kusema na moyo wa Anania na mkewe, chemichemi za uhai wake zilizima na ndani yake ikaanza kutoka sumu hata kufika hatua kusema uwongo na kumdanganya Roho Mtakatifu. Yeye na mkewe waliunza shamba lao la urithi, lakini kwa sababu shetani alishatia sumu moyoni mwao wakaleta kiasi pungufu cha fungu la kumi. Kwa sababu ya kujazwa sumu na Shetani alifanya jambo lisilo la kawaida na kumdanganya Roho Mtakatifu. Nakutangazia siku ya leo ikiwa umewekewa sumu ndani yako nina iharibu leo kwa jina la Yesu.
Matendo ya mitume 5:1-4 “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.”
Shetani akijaza sumu ndani ya mtu kuna mambo yanatokea, mambo hayo ni kama yafuatayo;
1. Kufanya mambo yasiyo ya asili yako
Utaona Petro anamwambia Anania, kwanini Shetani ameujaza moyo wako uwongo na kudiriki kumdanganya Roho Mtakatifu.
Kila jambo lolote ambalo si la kikawaida chanzo chake ni sumu ya Shetani. Ukiona mwanaume na mwanaume wanaoana fahamu chanzo chake ni sumu ndani ya moyo wao.
Sumu ikiingia ndani ya moyo wa mwanadamu ndipo utaona mtu anafanya maamuzi ya hovyo kabisa, anapoteza vitu vya thamani kwa pesa ndogo. Moyo unabadilika anafanya maamuzi ambayo siyo yake mwenyewe