PENUEL GLORIOUS MINISTRY OF TANZANIA

PGMT

ASKOFU WA KANISA LA PENUELI MAKAO MAKUU MPANDA KATAVI

Monday, October 13, 2025

SOMO:NEEMA YA MUNGU - 2

Jambo la Pili : Neema moja inaweza kukusaidia kuomba na kupata Neema zingine. Angalia kwenye Biblia; Kutoka 33:13 …Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. Musa alipokuwa anafanya maombi alisema kuwa, kama amepata Neema mbele za Mungu, 'apate neema mbele zake'. Ukisoma hiyo sentensi ina neno 'neema' mara mbili; yaani kuna 'neema' mbili tofauti zinazungumziwa kwenye mstari mmoja. Neema ya kwanza anayoitaja ni Neema ambayo inamsaidia kwenye kuomba vitu vingine. Ni msingi wa maombi yake, kwa sababu haanzi kuomba kwanza mpaka ameuliza kama ana Neema za kusongea mbele za Mungu ili kufanya maombi ya vitu vingine. Neema ya pili inayotajwa kwenye mstari ni ombi. Anaomba apate neema. Na ili apate hii neema ya pili lazima awe na neema ya kwanza aliyoitaja. Asipopata neema ya kwanza maana yake na Neema ya pili ataikosa. Neema ya pili ni ombi la yeye kutaka Mungu awe pamoja naye ili kuwaongoza wana wa Israel kuelekea Kanaani. Kwa hiyo neema moja inaweza kukusaidia kuomba neema nyingine. Si wengi sana wanaojua kuwa neema zipo nyingi. Kuna neema nyingi sana lakini ufunguo wa neema zote tunazopokea ni Yesu Kristo, maana ndiye aliyekuja na Neema na kweli (Yoh 1:17). Kwahiyo Neema ya kwanza inayoweza kukusaidia kuombea neema zingine ni Neema ya kuwa na Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako. Ndani yake yeye (Yesu) ndimo tunachota kila aina ya Neema, na ndio maana tunasema tupo kwenye kipindi cha neema na siyo kipindi cha sheria kama ilivyokuwa kwenye Agano la kale. Msingi wa Agano jipya ni neema. Yohana 1:16 …Kwa kuwa katika utimilifu wake {Yesu} sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Biblia ipo wazi, inasema katika utimilifu wake Yesu Kristo (alitimilika msalabani) tulipokea na neema juu ya neema. Kupitia msalaba wa Yesu kristo siyo tu kwamba tunapata neema, bali tunapata na neema juu ya neema . Maana yake kupitia msalaba unaweza ukapata neema nyingi tu. Neema ya kumwamini Yesu Kristo na kuamini alichokifanya msalabani ni mlango wa wewe kupokea neema zingine nyingi. Nachotaka uone pia ni kwamba neema siyo moja, zipo neema nyingi sana ambazo ziliachiliwa msalabani ni kazi yetu sisi kuzichukua. Ndiyo maana kwenye Biblia anasema 'tulipokea na neema juu ya neema'. Anatumia neno 'tulipokea' na siyo tutapokea. Anatumia wakati uliopita na siyo uliopo. Maana yake neema zilishakuja kupitia msalaba, siyo zitakuja, bali zilikuja! Ni swala la sisi tu kuzichukua msalabani tu. 2 Wakorintho 9:8 ….Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; Matendo ya Mitume 4:33 …Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote Ukisoma kwenye hiyo mistari utagundua kitu kwamba Neema zipo nyingi na wala haipo moja. Tupo kwenye kipindi cha Neema kwa sababu tupo kwenye kipindi cha kupitia utimilifu wa Yesu msalabani tulipokea Neema nyingi. Wakorintho inatwambia kwamba Mungu aweza kuwajaza kila Neema kwa wingi, Neno 'kila' linaonyesha kwamba zipo nyingi lakini Mungu anaweza kukujaza zote. Kama Mungu anaweza kutupa kila Neema basi na tupige magoti kwake atupe Neema / za kutosha. Kuna neema ya kumjua Mungu ;kuna neema ya kumtumikia Mungu ; kuna Neema ya kushiriki ibada, n.k Omba Mungu akupe Neema nyingi ili uwe kwenye kipindi cha neema kweli kweli, kuliko unatamba kwa watu kwamba upo kwenye kipindi cha Neema kumbe hata nini maana ya Neema hujui. Jambo la 3: Neema yako inaweza kuwabeba na watu wengine. Neema ipo kwa ajili ya kutufanya tuishi ndani ya kusudi la Mungu. Na kusudi la Mungu ni kwa ajili ya watu wa Mungu. Kwa hiyo unaweza ukapewa Neema wewe ila ikawasaidia na wengine! Angalia kwenye Biblia; 1 Petro 4:10 …kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. Biblia inatuonyesha kuwa kama mawakili wa Neema inatubidi tuwe tunahudumiana kwa kadiri ya karama ya kila mmoja wetu. Ni kama anataka kutwambia kwamba Neema uliyopata iliyokupa hiyo Karama itumie kwa ajili ya kuwahudumia wengine , Maana ukirudi kwenye jambo la kwanza nilikwambia kuwa NEEMA ya Mungu ndiyo inaonyesha kusudi/ huduma/ Karama ya Mungu kwenye maisha yako. Ukipokea neema ya Mungu itumie kuhudumia watu. Kutoka 33:16 ..Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? Musa aliomba Neema yeye pekee yake kwenye mstari wa 13. Kwenye mstari wa 16 anataka kujua kama Neema aliyoomba itawasaidia na wenzake? Maana yake Musa alijua kabisa kwamba akipata Neema yeye itawasaidia na watu wengine pia. Mwanzo 6:8 …Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA. Wasomaji wa Biblia wanajua kwamba Neema aliyoipokea Nuhu haikumsaidia yeye pekee yake, bali iliokoa uhai wa mbegu ya viumbe hai duniani na uhai wa watu nane, yaani Nuhu, hamu, yafethi na Shemu pamoja na wake zao; lakini hao saba hawakupata Neema isipokuwa Nuhu pekee yake, na kwa sababu hiyo wengine wote saba waliokolewa kwa faida ya Neema iliyokuwa kwa Nuhu. Ukipata Neema tambua kuwa ni kwa ajili ya watu pia. Mungu atusaidie. Jambo la 4: Unaweza ukawa na Neema ya Mungu lakini isijae. Neema ya Mungu ina kipimo chake, inaweza kujaa au kutokujaa. Sasa unaweza ukawa una Neema ya Mungu lakini ikawa haijajaa katika kiwango kinachotakiwa. Ngoja tuangalie kwenye Biblia alafu uone kitu huko. Matendo ya Mitume 6:8 ..Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Biblia inamtaja stefano kama mtu aliyejaa Neema. Kama Biblia imemtaja stefano kuwa alijaa Neema maana yake walikuwepo watu wengine ambao hawakujaa Neema, japokuwa walikuwa nayo. Je wewe umejaa Neema ya Mungu? Imani yako katika kristo ndiyo itaamua neema iweje ndani yako. Waebrania 12:15 …mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. Waebrania inatwambia kuwa mtu asiipungukie neema ya Mungu. Na anatoa ni tahadhari maana anaanza kwa kusema, mkiangalia sana, mtu asiipungukie neema ya Mungu; ni tahadhari hii. Kwa hiyo kama mtu hataangalia sana [ kama hatachukua tahadhari ] anaweza kujikuta ameipungukia neema ya Mungu kwa kujua au kwa kutokujua. Imani yako thabiti juu ya Yesu Kristo na kile alichokifanya msalabani basi ndiyo itakufanya uendelee kuwa na neema ya Mungu yote. Ukiugeuzia mgongo msalaba na Neema ya Mungu inaanza kupungua kwako. Tunapokea Neema kwa njia ya msalaba kupitia Yesu Kristo. Msisitizo upo kwenye kutambua kuwa inawezekana unaishi ukiwa na Neema ya Mungu lakini ikiwa ni ndogo sana; chukua tahadhari. INAENDELEA SEHEMU YA TATU

Saturday, October 11, 2025

SOMO : NEEMA YA MUNGU -1

SOMO : NEEMA YA MUNGU KITABU CHA SOMO: Warumi 12:6 …Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; Na Askofu Mkuu Dr. Burton Saulo Yuda. Maana ya Neema ya Mungu ni kipawa kutoka kwa Mungu au ni upendeleo unaokuja toka kwa Mungu kupitia Yesu kristo kwenye maisha yetu. Neema ya Mungu ni kitendo cha kustahili mahali ambapo hatukustahili. Ni kufaa eneo au mahali ambapo hatukufaa tuwe. Ni kipawa toka kwa Mungu mwenyewe kutupa kitu au vitu ambavyo hatukustahili. Mtu yeyote asijisifu kwa chochote kile. Vipo vitu kadha vya msingi kuvijua kuhusu Neema ya Mungu. Kwenye somo hili tutajifunza mambo saba muhimu ya kuhusu Neema ya Mungu. Jambo la kwanza : Neema inabeba kusudi la Mungu kwenye maisha yetu. Si wengi sana wanaojua kuwa unaweza ukaombewa au ukaomba kwa Mungu na ukapata Neema ya Mungu ambayo ulikuwa huna. Tuliangalia huko juu kuwa Mungu anaweza kutupa 'kila' Neema. 2 Wakorintho 9:8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema. Huu mstari unaonyesha wazi kwamba Mungu 'anaweza' kutupa kila Neema. Na kama Mungu anaweza kutupa 'kila' Neema maana yake kumbe tuna uwezo wa kusogea msalabani pake na tukapata Neema tunayoihitaji. Kumbuka Neema zimekuja kupitia utimilifu wa Yesu pale msalabani. Kwa hiyo kama tukitaka kupata Neema ya Mungu, na tuusogelee msalaba wa Yesu kwa imani ili tupate Neema zilizoachiliwa hapo msalabani. Kama unahisi hakuna Neema juu ya maisha yako muombe Mungu kwa imani nayo utaipata (kama ni kwa mapenzi Si watu wengi wanaofahamu kuwa kusudi la Mungu kwenye maisha yao limebebwa kwenye kitu kinachoitwa NEEMA YA MUNGU. Ngoja tuangalie maandiko uone; Warumi 12:6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani. Paulo a.navyowaambia warumi kwamba tuna Karama mbalimbali lakini kwa 'kadri ya Neema' tuliyopewa. Ile Neno 'kwa kadri' linaonyesha kipimo. Maana yake kipimo cha Karama tulizonazo ni Neema ya Mungu. Kama Neema ya Mungu ni kubwa kwako, hata Karama itakuwa kubwa pia. Kama Neema ya Mungu ni ndogo hivyo hivyo pia na Karama itakuwa ndogo; maana Karama ni kwa kadri ya Neema tuliyopewa. Tunajua kuwa Karama tulizopewa zipo kwenye kusudi la Mungu kutuumba na kutuweka duniani. Kwa hiyo kama Neema ya Mungu ndiyo kipimo cha Karama basi Neema ya Mungu inabeba kusudi la Mungu kwenye maisha yetu. Neema kubwa inabeba kusudi kubwa, Neema ndogo inabeba kusudi dogo. Lile Neno 'kwa kadri' linaonyesha kuwa viwango vya Neema vinatofautiana. Waefeso 4:7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. Angalia hapo kwenye waefeso jinsi Biblia inavyosema. Biblia inasema kwamba kila mmoja alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake kristo. Maana yake kila mmoja amepewa Neema kwa kipimo ambacho Yesu Mwenyewe alipenda kugawa au kumpa. Kwahiyo kuna watu wana Neema kubwa na kuna watu wana Neema kidogo, lakini si kwa sababu ya matendo bali ni kwa sababu ya kipawa chake Kristo. Nataka uone hiki kitu, Neema zinatofautiana. Na sio wengi wanaojua kuwa Neema zinatofautiana. na watu kutokujua kuwa Neema zinatofautiana basi kuna muda wale wenye Neema kubwa wanaona wenye Neema ndogo kama wavivu hivi; na wale wenye neema ndogo wanaona kama wao hawafai katika kazi ya Mungu; lakini haipo namna hiyo. Utofauti wa Neema unakuja kutokana na utofauti wa kusudi la mtu na Karama ya Mtu. Neema zingefanana maana yake wote tungekuwa na kusudi moja! Sasa kwa sababu makusudi ya Mungu kwa mwanadamu ni tofauti tofauti basi hata Neema tunapewa tofauti tofauti na kwa kipimo tofauti tofauti. Neema iliyo kwangu mimi mwalimu haiwezi kufanana na Neema anayopewa mwinjilisti au mchungaji. Ndivyo hata warumi 12:6 imetuambia. Vipo vipengele kadha nataka uvione kwenye hili jambo la kwanza. a. Kazi ya Neema ni kukupitisha kwenye kusudi la Mungu. Ili kujifunza hiki kipengele natamani tutazame mifano kadhaa. Mfano 1. Nuhu. Mwanzo 6:8 .. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA. Wasomaji wa Biblia wanajua kuwa mwanadamu wa kwanza kupata Neema kwenye Biblia ni Nuhu. Kwa wale ambao hawajapata Neema ya kusoma Biblia, Nuhu ni yule jamaa ambaye alijenga Safina wakati wa gharika, bila shaka umewahi kusikia habari zake. Nachotaka uone kwa huyu ndugu Nuhu ni kwamba, popote utakapoona pana Neema ya Mungu basi ujue kuna kusudi la Mungu. Ukipewa Neema tu inakupitisha kwenye kusudi la Mungu. Ngoja tuseme hivi, Mungu alivyoona maasi kwa mwanadamu yameongezeka alipanga kutoa adhabu kwa kutumia mvua kubwa iletayo mafuriko makubwa (gharika) lakini Mungu hakutaka kuharibu kusudi lake na viumbe hai kuijaza Dunia. Kw hiyo Mungu akawa anamtafuta mtu atakaye mbebesha hilo kusudi ili atunze mbegu za viumbe hai. Biblia inasema Nuhu akapata 'Neema'. Kumbuka tulikotokea, ukiona Neema ya Mungu mahali ujue kuna kusudi la Mungu. Kwa hiyo Neema aliyoipata Nuhu ilikuwa kwa ajili ya kusudi la kutunza mbegu za viumbe hai duniani ambalo Mungu alimpa huyu ndugu Nuhu. Neema ya Mungu inakupa kusudi la Mungu kwenye maisha yako. Je unaifahamu Neema ya Mungu kwako, na ina kusudi gani? Mfano 2. Mariamu. Luka 1:28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Mariamu alipewa salamu na malaika Gabrieli, salamu ilitaja Neema ya Mungu. Maana yake Mariamu alikuwa amepewa Neema ya Mungu, na kwa sababu neema ya Mungu inabeba kusudi fulani bila shaka hii Neema ya Mungu haikuwa bure pia, ilibeba kusudi ndani yake! Je unajua ni kusudi gani hilo? Luka 1:31…Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Kusudi lililobembwa kwenye Neema aliyopewa Mariamu ilikuwa ni kutimiza kusudi la Mungu la kumleta Yesu Kristo duniani ili aje aichukue dhambi ya ulimwengu! Ukipewa Neema na haujaielewa muulize aliyekupa Neema kama Mariamu alivyofanya. Aliuliza hii salamu ni ya namna gani? Alafu akapewa jibu. Mfano 3. Esta. Esta 2:17 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti. Esta alipata Neema machoni pa mfalme Ahausuero baada ya aliyekuwa malikia (Vashti) kuonyesha dharau kwa mfalme. Esta akapata neema kwa mfalme ya kuweza kuchukua nafasi ya malkia Vashti. Sasa nataka utazame katika jicho la Mungu, yaani Mungu anamwonaje Esta? Mungu alimbebesha kusudi kubwa sana Esta kwa ajili ya wayahudi. Mungu alikuwa anamwandaa Esta kwa kuja kuwatoa katika hatari ya kuuawa ambayo Hamani angeitangaza siku chache mbele. Kwa hiyo nataka ujifunze hiki, aliyesababisha mfalme Ahausuero ampe Neema Esta ni Mungu mwenyewe. Yaani hivi, Mungu alimpa neema Esta ili apate neema mbele ya mfalme ili kusudi la Mungu litimie. Kabla mfalme hajampa neema Esta, Mungu alikuwa tayari amekwisha kumpa Esta Neema ili kuwalinda wayahudi wasiuawe na Hamani. Kuna muda tunapata neema (upendeleo) kwenye mashule, maofisini au kazini sio kwa sababu maboss zetu wametupenda tu bali ni kwa sababu Mungu ametupa Neema yake kwa ajili ya kusudi analotaka litimie kwenye hiyo shule, au chuo, au ofisi n.k Usipojifunza kufanya kazi na Mungu popote ulipo utajikuta unapata Neema (upendeleo) mahali ulipo alafu ukabaki unashangaa tu, ukawa mzigo kwa Mungu badala ya kuwa msaada kwa Mungu kutimiza kusudi lake! Mfano 4. Paulo. Wagalatia 1:15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, Paulo anasema Mungu alimtenga tangu tumboni mwa mama yake, akamwita kwa 'neema' yake. Tunajua kuwa ni kweli Mungu alimtenga Paulo kwa ajili ya kazi yake. Kwa hiyo alimwita kwa NEEMA yake , Ni kama anataka kutwambia kwamba Neema ya Mungu ndiyo iliyobeba kusudi la yeye kutengwa toka tumboni mwa mama yake. Na neema hii ya Paulo ilikuwa kwa ajili ya kusambaza injili kwa mataifa (kwa watu wasio wayahudi) Nimekupa hii mifano ili uone na ujue kuwa Neema ya Mungu haiji bure, inakuja na kusudi la Mungu. b . Kiwango cha kuishi ndani ya kusudi la Mungu kunategemea kiwango cha Neema. Neema ya Mungu ina kipimo tofauti tofauti, inaweza kuwa kubwa au ndogo. Sasa, kiwango cha wewe kuishi ndani ya kusudi la Mungu ,Kunategemea sana kiwango au kiasi cha Neema uliyo nayo! Ukiangalia maisha ya Paulo na maisha ya petro au maisha ya Yohana yalitofautiana. Kitu kilichotengeneza utofauti wao ni kiwango na aina ya Neema waliyokuwa wamepewa. Ngoja tusome kwenye Biblia uone kitu; 1 Wakorintho 15:10 ..Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. Ukisoma kwenye huu mstari unaona vitu kadha ndani yake. i) Maisha ya Paulo yalitegemea Neema aliyopewa na Mungu. Ukisoma huu mstari unaona Paulo anawaambia wakorintho kuwa "nimekuwa hivi nilivyo kwa Neema ya Mungu". Maana yake Neema ya Mungu ndiyo ilimfanya Paulo awe Paulo ambaye tunamfahamu. Huenda angeendelea kuishi nje na neema ya Mungu Paulo angeendelea kuwa muuaji na mpinzani namba moja wa injili. Kwa hiyo kilichomfanya Paulo abadilike toka kuwa mpinzani wa injili mpaka kuwa mhubiri wa injili ni Neema ya Mungu. Alafu mbele ya huo mstari anasema "nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote (mitume 12); wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami". Paulo anachotaka tuone ni kwamba, ile huduma aliyoifanya, kazi yote aliyoifanya na jinsi alivyofanya kazi kuzidi hata wale mitume 12 waliokuwa na Yesu kila mahali; kuwa ni Neema ya Mungu. Si kwa elimu, si kwa akili, si kwa mali wala ujuzi bali ni kwa neema ya Mungu. Maana yake bila Neema ya Mungu asingekuwa jinsi alivyo. Swali nililojiuliza ni kitu gani kilitofautisha kazi aliyoifanya Paulo na mitume wengine? Biblia inatoa jibu kuwa ni Neema ya Mungu. Kwahiyo hata wewe maisha yako jinsi yalivyo ni kwa Neema ya Mungu. Mimi mwenyewe jinsi nilivyo ni kwa Neema ya Mungu. Ukielewa hivi itakusaidia sana. Nimeona watu wengi sana wakiwa wanaiga huduma na Karama za watu. Lakini hawajui kama Neema iliyo juu ya wale watu anaowaiga na Neema iliyo juu yake ni tofauti! Sasa ukitaka uharibu kazi endelea kung'ang'ania huduma ya mtu wakati mna neema tofauti kabisa. Hata hivyo unapata wapi ujasiri wa kumuiga mtu au kujifananisha na mtu? Watu wengi sana ambao somo la Neema ya Mungu limewapita pembeni (hasa vijana) huwa wanafanya huduma mda mwingine kwa kushindana. Au wanafanya huduma kwa kuiga, au kwa kujifananisha na fulani. This is foolishness! A spiritual ignorance! Neema ya Mungu ndio itakuelezea wewe huduma yako ipoje na watu gani utawahudumia na mipaka ya huduma yako ni ipi. Kazi ya Mungu hatushindani, hatugombaniani, wala hatuigi; tunafanya kwa NEEMA ya Mungu. ii) Neema ya Mungu inaweza kuwa ya bure. Kutoka kwenye mstari wa 1 kor 15: 10 tunaona kitu cha pili pale, kuwa; Neema ya Mungu inaweza kuwa ya bure. Paulo anasema: "na Neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure!" Kama Paulo alisema hivi maana yake kuna muda na kuna watu Neema ya Mungu ni bure kwao yaani haifanyi kazi. Unaijua hatari ya kuwa na Neema ya Mungu alafu ikawa ya bure? Ukiona unaishi maisha ambayo nafsi yako tu inakushuhudia kwamba kuna jambo unapaswa kulifanya kiroho au kimwili na umelinyamazia ujue Neema ya Mungu ni bure kwako. Neema ya Mungu kuwa bure kwako ni kuishi chini ya viwango vya kusudi la Mungu kwenye maisha yako. Kuna mtu alinitafuta akaniambia mtumishi ninaona deni kubwa sana moyoni mwangu. Nina huduma kubwa sana ambayo Mungu ananishuhudia ndani yangu lakini maisha ninayoishi ni tofauti kabisa na huduma yangu. Kama wewe ni sawa na huyu mtu basi ni kwamba Neema ya Mungu iliyo ndani yako haifanyi kazi sawa sawa. Inabidi uingie kwenye maombi ya toba na maombi ya kukusaidia kuanza kufanya kazi ya Mungu. Mungu ni mwaminifu, atakujibu. Au unaweza kwenda na sadaka madhabahuni na ukaombewa, maana neema ya Mungu unaweza ukaombewa na ukaipata. Kikubwa chunga sana, Neema ya Mungu isiwe bure kwenye maisha yako, kwa sababu ikiwa ni bure maana yake unakwamisha kazi ya Mungu. Na mti ambao hauzai hukatwaa na kutupwa mbali ili inayozaa ipate nafasi na hewa kubwa zaidi ili izae sana! Je unataka kukatwa? Waefeso 3:7 …Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. Paulo alifanywa kuwa mhudumu wa injili ‘kwa kadri ya kipawa cha Neema ya Mungu’. Kwa hiyo huduma na namna unavyotakiwa kufanya vinatokana na Neema ya Mungu. Siku moja kuna mtumishi aliniita na kuniambia jambo. Akaniambia kuwa mimi nina huduma kubwa sana na akasema anashangaa kuona naongea na kila mtu, yaani waliookoka, waislamu na wapagani vizuri kabisa, na akaniambia kuwa yeye hawezi kutengeneza urafiki na watu wa dunia wakati yeye ni mhudumu (alikuwa mwinjilisti). Nikamjibu kivyepesi sana nikasema, sisi wote ni watumishi wa Mungu, lakini utofauti wa huduma na aina ya maisha tunayoishi yanatokana na kiwango cha Neema ya Mungu ambacho hakiwezi kufanana, na kama Neema hazifanani hata maisha yetu hayawezi kufanana. Nikamwambia jinsi maisha nayoishi ya kuwa na marafiki bila kujali dini jinsi yalivyonisaidia kukutana na watu wenye shida mbalimbali za kiroho na nikaweza kuwasaidia tofauti na kama ningekuwa nabagua. Nikamwambia kuwa, mimi siwezi kuishi kama yeye na yeye hawezi kuishi kama mimi kwa sababu Neema zinatofautiana na kila penye neema pana kusudi la Mungu; kama ambavyo tumejifunza huko juu. Sasa sikuambii na wewe uwe na marafiki bila kujali hali zao za kiroho, Wakikupoteza shauri yako Maana neema hiyo niliyopewa huenda wewe huna. Ndio maana kwenye mazungumzo yetu sikumhukumu wala yeye hakunihukumu kwa sababu ukinihukumu ninavyoishi ni umeihuku Neema ya Mungu inayonifanya niishi hivyo. Muda mwingine watumishi wa Mungu wanatengeneza tumigogoro kwa sababu ya vitu vinavyotengenezwa na Neema ya Mungu. Ila sina maana kila ugomvi unatokea hapo, no! Nataka tu uone na ujifunze jambo. Jifunze hili somo la Neema ya Mungu itakusaidia sana. Mungu akusaidie uelewe zaidi ya hapa ili uweze kulifanyia kazi vizuri. Limekuja kwako kwa wakati wa BWANA kabisa. 2 Wakorintho 6:1 ..Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. Msisitizo upo kwenye 'msipokee neema ya Mungu bure'. Hapa nataka kukupa msisitizo kwenye lile jambo la pili kwenye kile kitabu cha 1 kor 15:10 kuwa NEEMA ya Mungu inaweza ikawa bure kwako. Kama Paulo anavyowasihi wakorintho na mimi pia nawasihi leo watanzania wenzangu na mlio nje ya nchi katika jina la Yesu kristo, msiipokee Neema ya Mungu bure. Ni wachache wamepata neema toka kwa Mungu, sasa na sisi wachache tuliopewa Neema ya Mungu tukiifanya iwe bure tunaharibu kazi ya Mungu aliyotupea Neema katika kusudi lake duniani. c. Neema ya Mungu inakufundisha namna ya kufanya na namna ya kuishi. Kutoka 33:13….Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. Musa aliomba kwamba kama amepata Neema mbele za Mungu basi Mungu amwonyeshe njia. Maana yake Musa alijua kuwa bila Neema ya Mungu asingeweza kupata njia! Ndio maana haanzi kuomba kuona njia bali anatanguliza kwanza kuomba NEEMA YA MUNGU, akiwa anajua kuwa Neema ya Mungu ikija itakuja na njia ya Mungu ndani yake. Musa baada ya maombi ya muda mrefu, alipata NEEMA mbele za Mungu na Mungu akaanza kumwonyesha njia ya kuwaongoza wana wa Israel kuelekea Kanaani. Kumbuka kuwa Musa aliingia kwenye haya maombi baada ya Mungu kughairi kuwaongoza na akataka atume malaika ndiye awaongoze kwenda Kanaani ndipo Musa alipoomba Neema ya Mungu. Sasa nataka uelewe kuwa Neema ya Mungu ndiyo inaweza kukusaidia kukuonyesha njia ya wapi upite kwenye kusudi Mungu aliloliandaa maishani mwako. Nimekuambia kuwa palipo na Neema ya Mungu pana kusudi la Mungu na kwa hiyo Neema haiishii tu kukupa kusudi bali pia inakupa njia ya kulifikia kusudi la Mungu kwenye maisha yako! Wengine wanatangatanga hawajui waanzie wapi kutimiza kusudi la Mungu, lakini jibu ni jepesi sana, ni kutafuta na kuomba NEEMA ya Mungu kama Musa alivyofanya. Neema ya Mungu ni ‘set’ kamili inayobeba vitu vyote unavyohitaji kuvijua kuhusu kusudi lako. Neema ya Mungu ni kama mwalimu anayekufundisha ili ufaulu mtihani, ndivyo Neema ya Mungu ilivyo. Angalia kwenye Biblia; Tito 2:11-12 .Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa’ Nataka uone hili neno 'nayo inatufundisha'. Neema ya Mungu inapokuja inakuja kukupa maelezo, au kukufundisha kitu gani cha kufanya. Hapo alikuwa anaongelea Neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu, ambayo inatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, n.k. Lakini linapokuja swala la Neema ya Mungu kwa ajili ya kusudi la Mungu duniani uwe na uhakika itakufundisha pia namna ya kuishi na kutembea kwenye kusudi la Mungu. Sasa unaweza ukaelewa kwa nini nimesema neema ya Mungu inakufundisha na kukuonyesha njia ya kuishi kwenye kusudi la Mungu. Mungu anapotaka kukupa Neema anakupa na maelekezo au mafundisho ili hiyo neema ikufundishe. Najua utaniuliza, atanipaje maelekezo na nitajuaje kuwa haya ndio maelezo ya neema ya Mungu? Ni rahisi sana, Mungu anakupa maelekezo ya Neema kupitia kitu kinachoitwa 'neno la Neema'. Angalia kwenye Biblia uone jambo. Matendo ya Mitume 20:32 ..Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. Biblia inazungumzia 'neno la Neema' Na mojawapo ya kazi ya hili 'neno la neema' ni kutujenga na kutupa urithi wa Rohoni. Maana yake Neno la Neema linapoachiliwa kwenye maisha yetu linabeba maelekezo ya kutujenga katika kusudi la Mungu na kutupa urithi wa Rohoni. Neno la Neema ni kama lile alilolipokea Mariamu alipokuwa anapewa ujumbe wa kumpata Yesu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Lilimsaidia kupambana na makwazo yote yaliyoinuka na kupinga kuzaliwa na kukua kwa Yesu. Mungu anakupa Neno la Neema kupitia Neno Lake Takatifu. Ndio maana ni muhimu sana kusikia Neno la Mungu kila linapokuja. Na ni vizuri zaidi kujifunza kuisikia sauti ya Mungu kwenye maisha yako kwa sababu inakupa maelekezo yote sawa sawaa na neema ya Mungu iliyo juu yako. Nakufundisha hili somo ili uweze kuomba na kutambua ni neema gani uliyonayo, na kuomba Mungu akusaidie kulitambua Neno la Neema kwenye maisha yako. Hakuna Muujiza mwingine wa kuijua neema ya Mungu na neno la Neema ya Mungu kama mahusiano yako na Mungu ni mabaya na kama hutajiingiza kwenye maombi ya kuomba juu ya Neema ya Mungu. INAENDELEA SEHEMU YA PILI

Tuesday, July 6, 2021

HATUA ZA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI

Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’ (1Timotheo 4:12 & 14). Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo. Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingereza la ESV unasema ‘Keep a close watch on yourself and on the teaching. Persist in this, for by so doing you will save both yourself and your hearers’. Kwa mujibu wa dictionary ya kigiriki na kiebrania neno ‘save’ lina maana ya kuweka huru (deliver), kulinda (protect), kuponya (heal), kutunza (preserve), kuokoa (save). Jambo muhimu ambalo Mtume Paulo alikuwa akilisisitiza hapa ni hili; jambo muhimu si tu kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako, bali kila mwamini ana kazi kubwa ya kufanya ili KUULINDA NA KUUTUNZA WOKOVU WAKE. Moja ya changamoto kubwa sana ambazo zinawakabili vijana wengi waliokoka leo ni kuipenda dunia. Kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana wengi na kwa sababu ya kuipenda dunia; (a) Mahusiano ya vijana wengi na Mungu wao yameharibika (b) Maisha ya vijana wengi yamekosa uelekeo (c) Kutokana na uovu wao jina la Bwana Yesu limekuwa likitukanwa. Katika kile kitabu cha 1Yohana 2:16 ni dhahiri kwamba dunia imejaa TAMAA YA MWILI, TAMAA YA MACHO NA KISHA KIBURI CHA UZIMA. Tamaa ina nguvu ya kuvuta pamoja na kudanganya, naam inamuingiza mtu kwenye jaribu. Hii ina maana tamaa ni mlango, naam mlango huu unapaswa kufungwa mapema usikupoteze. Hebu tujifunze kutokana na anguko la mfalme Daudi na mke wa Bathssheba (Samweli 11:1-2). Tunaona anguko la Daudi lilisaabishwa na kumpa Ibilisi nafasi kwa kutokwenda vitani. Mkristo akipoa katika kuvipiga vita vya kiroho inakuwa rahisi kwake kuanguka dhambini (Yakobo 1:14-15), naam kumbuka kwamba siku zote tamaa inalenga kumfurahisha mtu binafsi (self-pleasing) bila kujali matokeo yake. Hivyo katika nyakati tulizonazo sasa suala la kuipenda dunia ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa vijana wetu. Ujumbe huu mfupi unalenga kueleza kwa namna gani kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana na nini vijana wafanye ili kuikabili na kuishinda changamoto husika. Pia katika waraka 2Timotheo 2:15 Mtume Paulo anaendelea kumwambia kijana Timotheo ‘Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli’. Pengine kila mmoja wetu atafakari maisha yake kwa kuhusianisha na maelekezo ya Paulo kwa Timotheo. Naomba jiulize na kujijibu kwa uaminifu kwamba mosi, je, ujana wako wako unaheshimika au unadharauliwa? Pili, je, kwa waamini wenzako umekuwa kielelezo cha kweli kwa habari ya imani, upendo, usafi, usemi na mwenendo au la? Binafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwa namna gani kijana atahakikisha kwamba (a) Ujana wake haudharauliwi (b) Anakuwa kielelezo kwa waamini wenzake (c) Anathibitisha kwamba kweli amekubaliwa na Mungu. Naam katika kusoma na kutafakari neno la Mungu nimejifunza kwamba zifuatazo ni njia ambazo zitatusaidia sisi vijana wa leo kuifikia kweli hii ya neno la Mungu. • Kijana adumu katika kuomba na kusoma (kutafakari + kulitenda) neno la Mungu Katika Zaburi 119:9 & 11 Biblia inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii AKILIFUATA neno lako’. Pia kwenye ule mstari wa 11 inasema ‘moyoni mwangu nimeliweka neno lako, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI’. Naam katika Mathayo 26:41 imeandikwa ‘Kesheni, mwombe, MSIJE mkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu’. Yohana 17:17 inasema ‘uwatakase kwa ile kweli ;neno lako ndiyo kweli. Mambo haya mawili yanapaswa kwenda kwa pamoja nakijana akidumu katika kuomba na kusoma neno la Mungu ushindi ni lazima. • Kijana asimpe Ibilisi nafasi. Kijana anapaswa kujiuepusha na mazingira yenye kumfanya aiepende na kuifuatisha namna ya dunia hii. Katika kitabu cha 1Wakorinto 6:12 imeandikwa ‘Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote VIFAAVYO; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya UWEZO wa kitu chochote’. Ni vizuri ukahakikisha kwamba ufahamu wako hautawaliwi na mambo yasiyo ya msingi (non-essentials of life) – Je ufahamu wako umetawaliwa ni nini? Hii ndiyo sababu iliyomfanya Paulo awaambie Waefeso ‘Wala msimpe Ibilisi nafasi’ (Waefeso 4:27) na pia awaambie Warumi “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake’. Toleo la KJV linasema ‘But put ye on the Lord Jesus Christ, and MAKE NOT PROVISION for the flesh, to fulfill the lusts thereof’. Na toleo la ESV linasema ‘But put on the Lord Jesus Christ, AND MAKE NO PROVISION FOR THE FLESH, TO GRATIFY ITS DESIRES’ (Warumi 13:14). Je hivi leo ni kwa namna gani vijana wanaungalia mwili na kumpa Ibilisi nafasi? – Mitandao ya kijamii, kuangalia na kusoma vitu vichafu, hasira, mawazo, mazingira. • Kijana azikimbie tamaa za ujanani Katika 2Timotheo 2:22 imeandikwa ‘LAKINI ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi’. Kijana anawezaje kuzikimbia tama za ujanani? Hebu tuangalie mfano wa Yusufu. Ushindi wa Yusufu dhidi ya mke wa Uria (Mwanzo 39:2-9). Hii ni habari ya kijana Yusufu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mali za Potifa. Pamoja na ushawishi aliokutana nao Yusufu alijibu kwamba ‘Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?’ Mwanzo 39:12 inasema ‘huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake akakimbia akatoka nje. Ili kuzikimbia tamaa za ujanani kijana anapswa (a) ajiepushe na mazingira/marafiki wabaya (Mithali 1:10 & 1Wakorinto 15:33) (b) Ajitenge na uovu (Mithali 16:17, Zaburi 1:1). Ni muhimu ukakumbuka kwamba hukupewa mwili kwa ajili ya zinaa maana miili yenu ni ni viungo vya Kristo na tena hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 6:15 & 19), tena yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorinto 6:17) maana tena imeandikwa ‘Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili’ (1Wakorinto 6:13b). Tena imeandikwa ‘Lakini uasherati USITAJWE kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu’ (Waefeso 5:3). • Kijana ajifunze kuenenda kwa roho na si kwa mwili Katika wagalatia 5:16 imeandikwa ‘Basi nasema ENENDENI KWA ROHO, wala HAMTATIMIZA kamwe TAMAA ZA MWILI. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayoyataka’. Je kuenenda kwa Roho ndio kukoje? Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote (Yohana 16:13) na pia imeandikwa ‘kwa kuwa wote WANAOONGOZWA na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’ (Warumi 8:14). Kuenenda kwa Roho ina maana ya kuishi kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako (Warumi 8:2). Naam kadri unavyokuwa mtiifu kufuata utaratibu wake ndivyo unavyokuwa mbali na sheria ya dhambi na mauti ambayo ni mwili. Kumbuka imeandikwa ‘kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waiufuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani (Warumi 8:5-6) na pia Wafilipi 4:8. Naam imeandikwa ‘Kila mmoja wenu ajue KUUWEZA MWILI wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu HAKUTUITIA UCHAFU, bali tuwe katika utakaso’ (1Thesalonike 4:4-5, 7). Ni jambo la ajabu sana kwamba kwamba tumepewa fursa ya kuiweza miili yetu. Ndio tunapaswa kuuweza mwili kwa maana ya kuudhibiti kwa kuuongoza na kuufanya ufuate nia ya roho. Kijana mwenzangu kama umechagua kumpa Yesu maisha yako kwa njia ya wokovu, nakusihi na kukushauri zingatia haya ili kuwa na maisha yenye kielelezo na ushuhuda mzuri maana imeandikwa ‘Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa’ (2Petro 2:20-21). AMENI

Wednesday, June 30, 2021

SOMO: SUMU YA SHETANI KWENYE MOYO -2

2. Anabadilika badilika kwenye maamuzi yake Mtu ambaye ana sumu ya shetani moyo wake unatema mauti badala ya uzima. Wakati Wayahudi wanatafuta namna ya kumuua Yesu, ndipo shetani akamwingia Yuda na kisha akasema na wakuu wa makuhani akasema nao jinsi ya kumtia mikononi. Kwa hali ya kawaida mtu hawezi kumuuza baba yake, lakini baada ya kutiwa sumu Yuda alibadilika maamuzi yake na akaenda kujadiliana na wakuu na makuhani namna ya kumtia Yesu hatiani. Luka 22:3-4.. “Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.” Unakuta mtu anawazo zuri sana juu ya maisha yako na anakwambia nitakupa mtaji, nitakupa biashara lakini Shetani akimwingia anabadilika kabisa. Yuda alikuwa ni mtu mzuri kabisa anatunza fedha za huduma ya Yesu, lakini Shetani alipomuingia andipo akaanza kufanya maamuzi ya kumuuza Yesu. Yohana 13:2.. “Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti;” Sio kwamba shetani aliweka moyo mwingine ndani ya Yuda bali aliweka sumu kwenye moyo wa Yuda. Aliweka kitu cha usaliti, yaani uasi, ukawekwa kwenye moyo wa Yuda ndipo sasa akaanza kuwaza kumsaliti. Sumu ndio hiyo mipango ya usaliti. Ukiona mtu alikuwa na bidii kanisani tena amefika kuitwa Pastor, lakini gafla akaacha hata hasalimii njiani ujue Shetani ameweka sumu ndani ya moyo wake. Sumu ya Shetani inaharibu tabia za watu, unashangaa watu wawili wanafunga ndoa kanisani na walipooana waakaitana majina yote ya kimapenzi lakini gafla unashangaa mmoja anasema simpendi huyu, simtaki huyu. Ni kwamba Shetani ameweka sumu ndani yake, ikambadilisha moyo na mawazo yake. Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. Akamshawishi kwa maneno mengi lakini bada ya kulala naye akamchukia sana. Unajifunza kwamba unaweza kudanganywa kwa maneno matamu na kaka yule lakini baada ya kubali kulala naye anakuchukia machukio makuu. Wewe binti, usikubali kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa, hata kama unadanganywa kwamba atakuoa usifanye hivyo. 2 Samweli 13:14-15 “Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.” Linda sana moyo wako kuliko vyote ulivyonavyo, ukiona kijana unafanya tendo la ndoa kabla ya ndoa na anasali kabisa kanisani ujue moyo wake tayari umeharibika. Miaka ya nyuma mkristo kupata mimba kanisani lilikuwa ni jambo la aibu na kuogopa lakini siku hizi jambo hili limekuwa ni kawaida kabisa. Bibilia inasema ikimbieni zinaa (1Wakorintho 6:18) lakini utashangaa mtu unashikwa mkono unapelekwa hadi gest, unapelekwa hadi porini lakini bado unasema Shetani mekupitia. Na kwa sababu hiyo utaomba sana, utaimba sana kama huachi hayo huwezi kufanikiwa. Kuna wakati unaomba lakini macho ya Mungu hayakuoni, wala sikio lake halikusikilizi maombi yako. Ni kwa ajili dhambi zako zinafanya Mungu asikii maombi yako; unaweza kuwa wengi sana na Mungu akasikia kwa mtu mmoja na mwingine asisikie. Ni kwaajili ya moyo uliojaa sumu; Shetani anakujaza uongo hatimaye unafanya makosa na unasema Mungu ni mwenye rehema. Hakika huwezi kufanikiwa. 2 Nyakati 7:14-17 “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu;” 3. Mauti Ndani ya moyo zikiingia sumu uhai unaondoka. Shetani akijaza sumu vile vitu vinavyoleta uhai ndani yako vinakufa na sumu inajaa ndani yako inakuathiri wewe na watu. Sumu hii itakufanya kudanganyika na ukidanganyika moyoni na kufanya maamuzi yasiyo sawa hatima yake ni lazima utakufa. Sumu ikiingia ndani yako hata kama upo salama leo siku moja utakufa mambo yako yatakufa, kazi yako itakufa kila kitu chako kitakufa. Matendo 5:5-11.. “Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya…. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.” 4. Anafanya vitu ambavyo sio hiari yake Kuna vitu unafanya sio kwa hiari yako, Shetani anasababisha ufanye si kwa nguvu zako. Shetani akiingia ndani ya moyo anakulazimisha. Kuna mambo unafanya ingawa ni mabaya lakini unayafanya kwa sababu Shetani ametia sumu kwenye moyo wako na hutendi kama wewe na kwa maamuzi yako, si kwahiari yako. Warumi 8:19-20 “Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha katika tumaini” Ukisikia habari za yule mtu ambaye alikuwa anakaa makaburini, ameacha nyumba yake na ndugu zake na kisha kuamua kuishi makaburini. Alikuwa anakimbizwa hadi jangwani kwa nguvu za pepo. Ndipo sasa unaona mtu anakimbia mume, anakimbia mke, anakimbia biashara kwa nguvu za pepo. Luka 8:29.. “Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo.” Watu wengi wamefeli masomo, wameshindwa kazi, wameacha ndoa ukimuuliza anasema nimesikia moyo wangu unasema, nimesikia roho mtakatifu anasema na mimi. Huyo sio roho mtakatifu ni roho mtakafujo. Roho mtakatifu hawezi kukutenga na watu, hawezi kuvunja ndoa yako. Unahitaji moyo wako uwe salama siku zote kwa maana moyo ukijaa sumu fikra zako zina haribika. Ndipo unaona mtu alikuwa anamsifia sana mume wake lakini gafla sasa anamchukia sana kuliko chochote, hawezi kuizuia wala kuitawala nafsi yake. Hawezi kuizuia nafsi yake, unamwambia mtu kabisa tabia hii ni mbaya uiache lakini hawezi kuacha kwa sababu hawezi kujizuia; moyo wake umejazwa sumu. 1Timotheo 5:6.. “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.” Ukiona umekuwa mgumu sana na utoaji kanisani ujue moyo wako umejazwa sumu, ni sawa na vile Anania na mke walipatana kumdanganya Roho Mtakatifu. Sio wewe ufanyae bali sheria ya dhambi ikaayo ndani yako, yale mambo unayapenda huwezi kuyafanya lakini yale ambayo hutaki kuyatenda ndio unayatenda. Ndani ya moyo wako umejazwa na mambo ya mabaya; ndio maana unawaza na kutenda mabaya. Leo Bwana akuponye kwa jina la Yesu. Moyo ukipata madhara, yale unayoatenda si wewe bali ile sumu ikaayo ndani ya moyo wako; kuna maamuzi umefanya ambayo sio sawa, ni ya maamuzi yaliyoathirika na sumu ya Shetani. Moyo wako ukihuishwa na uahi ukabaki ndani yako utafanya yale mazuri, hakuna atayakulazimisha kwenda kanisani, hakuna atakayekulazimisha kutoa kwajili ya Bwana utajikuta unafanya mwenye kwa kupenda.

SOMO: SUMU YA SHETANI KWENYE MOYO WA MWANADAMU -1

KITABU CHA SOMO. Matendo 5:3-4.."Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.” Na Askofu Burton Saulo Yuda wa Kanisa la Penuel Mpanda Utangulizi Wakati unataka kujifunza somo hili kuna vitu unapaswa kujiuliza; kwamba ni kweli Shetani anaweza kuujaza sumu moyo wa mtu ? na Je anaweza kuujaza sumu moyo wako wewe? Je ni kweli Shetani anazo sumu za kumjaza mtu? Je Shetani anaujaza moyo mambo gani ambayo ni sumu? Je, vitu hivyo vinavyoitwa sumu vinafaida au hasara? Mwisho wa somo hili moyo uliojaa sumu ili ufe Bwana anaenda kuuganga tena kwa jina la Yesu. MOYO KUJAZWA SUMU NA SHETANI Kabla sijakuelezea ni namna gani Shetani hujaza sumu na kwa njia gani, ngoja nikueleze kidogo kuwa Shetani ni nani. Shetani kwa asili anajulikana kama ni mwizi; huyu anayejaza watu sumu anafanya kazi kuu tatu kwenye maisha ya watu, kwanza ni mwizi. Wakati wowote aonekanapo huja kwa lengo lake la kuiba. Kazi yake ya pili ni kuua yaani aonekanapo popote huja kwa lengo la kuondoa uhai kwenye maisha ya watu na kazi yake ya tatu ni kuharibu, yaani akija kwenye maisha ya mtu huja kwa lengo la kuharibu kila kitu alichonacho. Imeandikwa; Yohana 10:10.. “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Mahali pengine Shetani anaitwa Mharabu. Sio muharabu yule wa Dubai unayemjua kuwa ni mweupe kwa sura, hapana. Mharabu huyu kwa kiingereza anaitwa Destroyer au mwenye uwezo wa kuharibu. Kwa Kiswahili cha kwaida angeitwa muharibu lakini kwa kiswahili fasaha anaitwa Mharabu na lengo lake ni kuharibu kila kitu masomo kazi, ndoa, biashara n.k. 1 Wakorintho 10:10… “Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.” Mahali pengine Shetani anajulikana kama muongo na na baba wa uongo. Shetani ni mshawishi wa mambo maovu anashawishi watu hadi wanaharibikiwa. Aliwahi kumshawishi mfalme Daudi kuwahesabu wana wa Israeli kinyume na mapenzi ya Mungu akasababisha Daudi kumkosea Mungu. Shetani akikushawishi unathiriwa moyo na hatimaye unaanza kutenda mambo ambayo si sawa. Shetani mahali pengine anajulikana kama mpanzi wa mambo mabaya kwenye Maisha ya watu. Anaweza kutia vitu vibaya kwa mtu na likakua kama pando baya na hatimaye maisha ya mtu yakaharibika kabisa. Ndio maana Bwana Yesu akasema kila pando lisilopandwa na Baba wa mbinguni litang’olewa kwa sababu Shetani naye hupanda mabaya kwa watu. Shetani anaweza kumtia mtu kifafa, anaweza kutia mtu ujinga, magonjwa n.k. Mathayo 15:13.. “Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.” Kwa sababu hiyo Shetani anaweza kuingia kwenye maisha ya mtu kwa makusudi mengi kama nilivyokueleza. Anaweza akaja kama mtu na kusema nawe na kisha kukupandia au kukutia sumu. Shetani anaweza kuongea na mtu na akisha sema naye roho ikamuingia. Kama aliweza kufika kwenye kiti cha enzi cha Mungu na akaanza kusema na Mungu (Ayubu 1:6-7) anaweza pia kumsemesha mtu sumu ikamuingia na mipango ya maisha yake ikaaanza kuharibika. Kwaajili ya kusemeshwa na Shetani ndipo utaona mtu alikuwa na juhudi kwaajili ya mambo ya Mungu gafla anaacha. Neno moja alilolisikia kwa Shetani likaharibu moyo wake na akaanza kuacha mambo yake ya msingi, akaanza kufanya maamuzi mabaya hatimaye anaharibikiwa. Shetani anaweza akaja kama Rafiki lakini kumbe ni yeye katika umbo la kibinadamu ili usijue. Mahali unapoishi mambo yako yameanza kuharibika, upendeleo wako kati yako na Mungu, na watu umepungua sana kwa sababu ya ile sumu iliyokuingia. Yule aliyekusemesha ukabadilika moyo wako ukaacha kumtumikia Mungu, ukaacha huduma, ukamuacha mke wako/ ukamuacha mume wako huyo aliyekusemesha sio mtu hata kama unakaa naye chumba kimoja ni Shetani kwenye mwili wa mtu. Kama vile Mungu akikusemesha roho inakuingia na kukusimamisha vile vile Shetani akikusemesha roho inakuingia na kukuangusha. Unaweza kusemeshwa ukaharibikiwa na kukosa imani juu ya Mungu na ukafanya mambo ya ajabu. Yale maamuzi uliyofanya ukamuacha mke wako/mume wako siku hizi uko single unahaha ni kwaajili ya moyo wako kujazwa sumu. Miaka yote mlikuwa pamoja mkipendana na kuitana kila aina ya majina ya mapenzi imekuwaje leo unampiga, unamtukana? Ni kwa ajili ya sumu ya Shetani. Unakuta mtu ni mlokole kabisa lakini anakuja kwa mwenzake anamwambia uache kusali, unajiuliza ni mtu huyu kweli? Sio mtu ni shetani katika umbo la binadamu. JINSI YA MOYO UNAVYOTIWA SUMU Moyo ni kituo kikuu (centre) cha maisha ya mtu ya kiroho na kimwili. Moyo ndio unabeba mambo yako yote ya kimwili na kiroho. Moyo ndio unawakilisha uhai wa asili wa mtu au ni chemichemi ya uhai wa mtu. Ndani ya moyo ndiko unapata uhai. Ndio maana bibilia ianasema linda sana moyo wako kuliko chochote. Sehemu nyingine moyo unawakilisha uamuzi wako au fikra zako hivyo ni kitu cha msingi kuliko vyote. Mithali 4:23… “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mungu anaagiza kwamba moyo wako unapaswa kulindwa kuliko kitu chochote. Kama kungelikuwa na uwezo wa kutumia silaha, basi unapaswa kuchukua bunduki kubwa na kuulinda moyo wako. Anasema linda sana moyo wako kuliko mke wako, kuliko mume wako, kuliko fedha au gari lako. Jiulize mbona wanajeshi hulinda mipaka ya nchi na raia wote, kwanini wewe hulindi moyo wako? Nakukumbusha leo kwa jina la Yesu unapaswa kulinda moyo wako kuliko yote uyalindayo. Shetani akishatia sumu kwa watu, unashangaa mtu anamwambia girl friend wake au boy friend ninakukabidhi moyo wangu? Jinsi gani asivyothamini moyo wake na hatimaye anapata matatizo makubwa. Unamsikia mtu anamwambia mwenzake kaa hapa nikueleze siri zote za moyo wangu, huyu athamini moyo wake kabisa. Bibilia inamtaja Samson kwa kosa lake kueleza siri zote za moyo wake na matokeo yake alitobolewa macho na kuteswa. Unajifunza usipolinda moyo wako kwa kusema kila kitu kilichomo ndani yako utatobolewa macho. Unashangaa magari yanalindwa, mashamba yanalindwa kwa alarm za bei kubwa kwa nini sasa moyo wako hauna ulinzi. Unatakiwa kuweka makombora kulinda moyo wako. Moyo usiokuwa na ulinzi utajazwa sumu na Shetani. Na Shetani akijaza sumu moyo wako hakika utaaribu ndoa yako, utaaribu kazi yako, utaaribu maisha yako na kila kitu chako kitaharibika . Moyo usipolindwa kuna chemchem za sumu zinaanza kuingia ndani yake. Sumu hizi huingia kwa njia nyingi hasa kwa kupitia maneno. Kuna mtu akikusemesha hakika mdomoni mwake inatoka sumu na ikikuingia moyo wako wote unaharibika. Unaweza kuambiwa jambo na mtu gafla ukaanza kumchukia mtu na tabia yako ikaharibika ukawa mtu wa tofauti kabisa, hivyo linda sana moyo kuliko vyote uvilindavyo. Shetani haangaiki sana na pua yako wala miguu, anahangaika na moyo ili pale uzima unapotoka patoke mauti. Unaweza ukawa umeokoka, ukaacha moyo wako bila ulinzi hakika utaharibikiwa. Mtu akisema na wewe angalia sana maneno yake maana yanaweza kuwa sumu kwako. Kuna vitu unafanya kwa hasira, uchungu kwa sababu kuna vitu vimekaa kwenye moyo wako kama sumu, leo Bwana akuponye kwa jina la Yesu. Baada ya Shetani kusema na moyo wa Anania na mkewe, chemichemi za uhai wake zilizima na ndani yake ikaanza kutoka sumu hata kufika hatua kusema uwongo na kumdanganya Roho Mtakatifu. Yeye na mkewe waliunza shamba lao la urithi, lakini kwa sababu shetani alishatia sumu moyoni mwao wakaleta kiasi pungufu cha fungu la kumi. Kwa sababu ya kujazwa sumu na Shetani alifanya jambo lisilo la kawaida na kumdanganya Roho Mtakatifu. Nakutangazia siku ya leo ikiwa umewekewa sumu ndani yako nina iharibu leo kwa jina la Yesu. Matendo ya mitume 5:1-4 “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.” Shetani akijaza sumu ndani ya mtu kuna mambo yanatokea, mambo hayo ni kama yafuatayo; 1. Kufanya mambo yasiyo ya asili yako Utaona Petro anamwambia Anania, kwanini Shetani ameujaza moyo wako uwongo na kudiriki kumdanganya Roho Mtakatifu. Kila jambo lolote ambalo si la kikawaida chanzo chake ni sumu ya Shetani. Ukiona mwanaume na mwanaume wanaoana fahamu chanzo chake ni sumu ndani ya moyo wao. Sumu ikiingia ndani ya moyo wa mwanadamu ndipo utaona mtu anafanya maamuzi ya hovyo kabisa, anapoteza vitu vya thamani kwa pesa ndogo. Moyo unabadilika anafanya maamuzi ambayo siyo yake mwenyewe

Saturday, May 23, 2020

MAKANISA MAPYA YA FUNGULIWA

Askofu Mkuu amefungua matawi mapya 20 katika mikoa ya Tabora, Shinyanga ,Mwanza,Mara na Simiyu.
endelea kuombea kazi hizi mpya

Tuesday, February 18, 2020

MASOMO YA KILA SIKU


Na bishop burton saulo yuda

Tutaenda kuangalia maana fupi ya maombi na matokeo ambayo mwamini huyapata kupitia maombi.

(i)  kupitia maombi mwamini anakuwa na uwezo wa kusoma Neno.
(ii) Mahusiano ya karibu na Mungu hujengwa.
(iii) Majukumu ya ki-Mungu uyapokea.
(iv) Humwezesha mwamini kushinda majaribu.
Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu
au ni mazungumzo Ambayo hufanyika  baina ya mwanadamu na Mungu.
Yeremia 33:3”Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua’’
Tambua Mungu ni roho.
MWANADAMU---------{MAOMBI}----------MUNGU
MUHIMU: Tambua mawasiliano yanayo fanyika baina ya mwanadamu na Mungu  ni tofauti sana na mawasiliano ya kawaida kwasababu.
(i) Mawasiliano ya kawaida hutumia mirango mitano ya fahamu.
(ii) Mawasiliano ya kawaida  unapo wasiliana na mwingine na yeye anapo jibu hapo ndipo mawasiliano huanza. Unapo mwomba Mungu haya ni Mawasiliano  ya Upande mmoja  kwa wakati huo wa kupeleka hoja zetu. Isaya 41:21”Haya,leteni maneno yenu,asema Bwana; toeni Hoja zenu zenye Nguvu, asema mfalme wa Yakobo.”
Mwamini huweza kutambua kama mawasiliano baina yake na Mungu  kama yapo vizuri pale tu Amani moyoni Inapo tawala wakati wa kufanya maombi. Pale mwombaji anapo omba na Moyoni mwake anakosa Amani hapo tambua kuna mambo mawili ya Msingi,yawezekana hayupo safi au yupo safi lakini shetani huweza kumsonga mwombaji na kumshuhudia uongo na kusababisha amani kutotawala vizuri.  Mwombaji huweza pokea majibu ya maombi yake kupitia;-
mawazo mapya, Unabii, Ndoto, Neno,Yohana 1:1,15:7,17:17, Zaburi 119:105.

FAIDA /UMUHIMU UNAOPATIKANA KUPITIA MAOMBI
(i) Humwezesha mwamini kusoma Neno.kupitia  maombi  mwamini  huweza kupata nguvu ya kusoma Neno  la Mungu kwasababu Mungu  hutumia Neno kutujibu mahitaji yetu tuliyo yapeleka kwake.kupitia Neno la Mungu,huweza kutuonya,kutufariji na kutuelekeza.Faida kubwa tunayo pata ni kwamba Roho Mtakatifu ndiye Anaye tusaidia kulijua  Neno baada ya kumwomba Mungu.1Timotheo 2:1
Ebrania 4:12”Maana Neno la Mungu li hai,tena lina Nguvu, tena lina ukali kuliko upanga  uwao wote ukatao kuwili, tena  lachoma  hata  kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta  yaliyo  ndani yake; tena  li jepesi kuyatambua  mawazo na  makusudu ya moyo.’’  Shetani  huweka vizuizi vikubwa sana kwa waamini katika swala la kupata muda wa maombi na kusoma  Neno. Pia yapo mahusiano makubwa sana kati ya vitu hivi viwili Maombi na Neno kwasababu Maombi bila Neno hayana nguvu pia kusoma Neno bila ya kumwomba Mungu akufundishe hakuna faida pia. Neno ni chakura cha mwamini pasipo Neno hakuna kukua  kwasababu mtu wa ndani hudumaa anapo kosa Neno/chakula na hupelekea kufa.
(ii) Mahusiano ya karibu na Mungu hujengwa.Mawasiliano hukuza Mahusiano kwa hiyo kupitia maombi mahusino makubwa huzaliwa baina ya Mwamini na Mungu .mfano katika hali ya kawaida kabisa  Inajulikana pale ambapo mahusiano  ya watu yanapo kuwa mazuri zaidi ndipo watu hawa huwa karibu sana .lakini pale ambapo hakuna maweasiliano pia mahusiano huwa mabaya ambapo watu hawa hawawezi kujuana vizuri kwa undani ukiringanisha na wenye ukaribu.Ndivyo hivyo kwa Mungu ,Mahusiano huwa makubwa  sana hata mwamini kutambua  siri nzito kutoka kwa Bwana ni pale tu ambapo mahusiano yanapo kuwa makubwa.Mungu huachilia siri/maelekezo mengi kwa Yule mwamini Ambaye yuko naye karibu sana.soma 1samweli 3:10,Daniel 9:21.
(iii) Majukumu ya k i-Mungu huyapokea. Ipo siri kubwa sana juu ya mawasiliano[maombi]  kati ya mwamini na Mungu, kupitia Maombi Mungu huachilia majukumu  yakufanya  kwa mwamini.
mfano ; Samweli , Musa ,Yakobo. Yakobo-kupitia ndoto Mungu aliachilia majukumu mengi kwa mtumishi wake huyu. Ibrahimu, Mwanzo 22:1-4,
Mungu alimpa majukumu ya kufanya Ibrahimu pale alipo kuwa na mawasiliano mazuri naye.hata wewe Mtu wa Mungu tegemea kupewa majukumu mengi zaidi endapo tu utadumisha na kukuza mahusiano na Mungu. Musa, kutoka 3:4-10.mtumishi wa Mungu huyu alipo kuwa na mahusiano mazuri na Mungu kupitia Maombi Mungu alimweshimu na kumpatia majukumu ya kufanya.rejea mstari wa 10;Mungu alimpa majukumu  mtumishi wake Musa baada ya kukubali na kuonesha nia  ya kweli katika upande wa mawasiliano.Note;Mjukumu wakati wote  mtu huweza kupewa kulingana na umri alio nao.hasa katika uwezo wa kiakili.swali je,anaweza kutunza siri na kumbukumbu vizuri,vivyo hivyo katika Mambo ya Ki-Mungu,Mungu huachilia  majukumu kwa waamini kulingana na kiwango cha kiroho cha mtu husika.Waefeso 3:20. Kiwango chako cha nguvu za Mungu zilizopo ndani yako huwa sababisho kwa Mun gu kuachilia mambo makubwa au madogo.Mwanzo 18:16-17.
(iv)  Humwezesha Mwamini kushinda Majaribu.
kupitia mahusiano mazuri na Mungu kwa njia ya maombi  Mungu huweza kumwonekania mwamini kwa namna ya tofauti sana pasipo hata yeye kujua. Zaburi 50:15.‘‘Ukaniite siku ya mateso,nitakuokoa, na wewe utanitukuza’’.
Bwana mwenyewe anathibitisha  kuwa kupitia mawasiliano(maombi)utamwita nay eye atakuokoa katika hilo jambo ambalo utakuwa unapitia.
Ayubu 22:27-30; Utawasiliana na Mungu na yeye atakusikia,kupitia maombi  mipango na ratiba  Bwana ataionesha  hata kama changamoto zitakuja  lakini  Bwana atakuvusha  na kukuinua  tena  katika kusudi lako.
Zaburi 22:23-24. Bwana anapenda mawasiliano yetu na yeye yawe katika  uhusiano ulio safi kabisa na hakika Mungu lazima Afanye.
MUHIMU: Kama ilivyo katika maisha  ya kawaida watu wawili wanapo kuwa karibu ndipo huanza kujuana kwa undani sana mfano,mambo ya kufahamu,kimahusiano  na kimichezo.
kama hawana  mahusiano usitegemee  kujuana kwa undani zaidi but juu juu tu.kiroho lazima ifike  sehemu kama kanisa la kristo tuamke na kumtambua Mungu  wetu kwa namna hii.Mungu anahitaji uhusiano mkubwa na sisi ili aweze kuachilia  majukumu mbalimbali ndani yetu ya kufanya.