KITABU
CHA SOMO: Mwanzo 12: 1-2…Bwana akamwambia
Abramu, toka wewe katika nchi yako ,na jamaa zako ,na nyumba ya baba yako ,uende
mpaka nchi nitakayokuomyesha .Nami nitakufanya wewe kuwa Taifa kubwa ,na
kukubariki na kulikuza jina lako ; nawe
uwe baraka.
Na: Askofu Burton Saulo Yuda wa kanisa la Penueli [ T ]
1.
UTANGULIZI.
Popote unapoona kazi ya Mungu imesonga mbele na kufanya
vizuri lazima kuna kiongozi aliyesimama kwenye nafasi yake vizuri.
Imekuwa ni tabia ya Mungu mara zote kumchagua mtu ili
kuyafanikisha malengo na mipango yake.
Mfano:
Mfano:
a)
Mungu alimuandaa Ibrahimu na kumwita
ili kuanzisha Taifa
b) Akamwandaa Yusufu ili kulihifadhi Taifa hilo Mwanzo 45: 3 -
9, 50: 20 - 21.
c)
Akamwandaa Musa ili kulitoa Taifa
hilo Utumwani - Kut.3:2-14.
d) Akamwandaa Joshua kuliongoza Taifa hilo kuteka nyara,
kupigana vita na kuliingiza Kanani - Yoshu 1: 1 - 9.
e)
Mungu alitumia wanaume na wanawake
katika kufikia malengo yake kama vile Nabii Debora - Amuzi 4:4, Esta 7: 3 - 6
n.k.
f)
Pia Mungu aliwaongoza na kuwaelekeza
waamuzi na wafalme katika kulisimamia kundi lake (watu) la Mungu, pia
aliwatumia Manabii ili kuwaonya na kuwasahihisha watu wa Mungu;
g) Na hatimaye alimtuma mwanaye wa pekee mpendwa Yesu Kristo
kuja kufa na kufufuka kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu kutoka katika utumwa wa
dhambi - Yoh. 3:16, Math. 1:21.
h) Yesu naye alipoondoka akamtuma Roho Mtakatifu ili atuongoze
salama - Yoh. 14: 16,26, Rumi. 8:14
Jambo la pekee katika ufalme wa
Mungu, mtu mmoja anaweza akaleta/akasababisha ushindi mkuu katika kanisa au
Huduma.
Hii ni ajabu Mungu anasema katika Ezek. 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakaye tengeneza boma, na kusimama
mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini
sikuona mtu.”
Kumbuka:
Hitaji kubwa la nyakati zote tangu vizazi na vizazi, katika watu wa kada zote, jamaa, Taifa, Mataifa, Taasisi na Mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza wengine,
Kumbuka:
Hitaji kubwa la nyakati zote tangu vizazi na vizazi, katika watu wa kada zote, jamaa, Taifa, Mataifa, Taasisi na Mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza wengine,
pia wenye uwezo na hekima katika
kuwaunganisha watu ili kuwafanya kuwa wamoja katika kutumia karama, vipawa,
talanta, huduma na rasilimali walizonazo kwa manufaa ya maendeleo yao. Pia
waweze kufikia na kukamilisha jambo/malengo na mipango yao waliyokusudia.
Viongozi wanajua wanalopaswa kulifanya na wana uwezo
Viongozi wanajua wanalopaswa kulifanya na wana uwezo
2.
MAANA YA UONGOZI.
Marko.10:45, 1Petr.2:21, Yoh.10:10 –
11
Uongozi ni hali/tendo la kuongoza.
Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani. na kuwachukua watu mbele zaidi ya pale walipo sasa .1Tim.4;11 - 12, 1Petr.2:21.
Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo.
Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (kushawishi) wengine wamfuate.
Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani. na kuwachukua watu mbele zaidi ya pale walipo sasa .1Tim.4;11 - 12, 1Petr.2:21.
Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo.
Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (kushawishi) wengine wamfuate.
Ni mtu aliyepewa dhamana (aliyeaminiwa) na Mungu kuongoza watu wengine (kuwatumikia). Mfano: Yesu - Yoh.14:6; 10:2 - 4, Paulo - 1Kor.11:1; 4:16.
Ni mtumishi (mtumwa) wa wale anaowaongoza.
Mfano: Musa - Kut.10:25 - 26; 13:21 - 22, Yuda - Mw.46:28
Kumbuka:
Kiongozi wa Kiroho siyo mtawala (boss) bali ni mtumishi (mtumwa).
Kiongozi ni kielelezo (mfano) wa kuigwa na, kufuatwa na wengine – Mfano Unaosimama mbele yao kuwaongoza.
Hivyo maisha ya kiongozi lazima yawe kielelezo katika maeneo makuu matano:-
A.
Katika Usemi:
Chunga (angalia) sana matumizi ya ulimi (yale uyasemayo). Yakobo 3:1 - 12.
B.
Katika Mwenendo:
(Tabia) - Maisha yako ya kila siku machoni pa watu. Math.5:16, 1Petr.2:11 - 12, Fil.2:14- 16.
C.
Katika Upendo:
Kujitoa, kujali, kuhudumia na kuhurumia. Yoh.3:16,
Math.9:35 - 38.
D. Katika Imani: Maisha ya kumtegemea Mungu. Ebr.10:38; 11:1,6, Hesabu.14:11, Yer.17:5 - 8, Rumi.1:17, Gal3:11.
E. Katika Usafi: Maisha Matakatifu - yenye ushuhuda mzuri mbele za watu. Zaburi.16:3, Kumb.23:14, 1Kor.3:16 - 17,
1Petr.1:16.
Somo litaendelea wiki ijayo .....