Na bishop burton saulo yuda
Tutaenda kuangalia maana
fupi ya maombi na matokeo ambayo mwamini huyapata kupitia maombi.
(i) kupitia maombi mwamini anakuwa
na uwezo wa kusoma Neno.
(ii) Mahusiano ya karibu na Mungu
hujengwa.
(iii) Majukumu ya ki-Mungu uyapokea.
(iv) Humwezesha mwamini kushinda
majaribu.
Maombi ni
mawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu
au ni mazungumzo Ambayo
hufanyika baina ya mwanadamu na Mungu.
Yeremia 33:3”Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa,
magumu usiyoyajua’’
Tambua Mungu ni roho.
MWANADAMU---------{MAOMBI}----------MUNGU
MUHIMU: Tambua mawasiliano yanayo fanyika baina ya mwanadamu na
Mungu ni tofauti sana na mawasiliano ya kawaida kwasababu.
(i)
Mawasiliano ya kawaida hutumia mirango mitano ya fahamu.
(ii)
Mawasiliano ya kawaida unapo wasiliana na mwingine na yeye anapo jibu hapo ndipo
mawasiliano huanza. Unapo mwomba Mungu haya ni Mawasiliano ya
Upande mmoja kwa wakati huo wa kupeleka hoja zetu. Isaya 41:21”Haya,leteni
maneno yenu,asema Bwana; toeni Hoja zenu zenye Nguvu, asema mfalme wa Yakobo.”
Mwamini
huweza kutambua kama mawasiliano baina yake na Mungu kama
yapo vizuri pale tu Amani moyoni Inapo tawala wakati wa kufanya maombi. Pale
mwombaji anapo omba na Moyoni mwake anakosa Amani hapo tambua kuna mambo mawili
ya Msingi,yawezekana hayupo safi au yupo safi lakini shetani huweza kumsonga
mwombaji na kumshuhudia uongo na kusababisha amani kutotawala vizuri. Mwombaji
huweza pokea majibu ya maombi yake kupitia;-
mawazo
mapya, Unabii, Ndoto, Neno,Yohana 1:1,15:7,17:17, Zaburi 119:105.
FAIDA
/UMUHIMU UNAOPATIKANA KUPITIA MAOMBI
(i) Humwezesha mwamini kusoma
Neno.kupitia maombi mwamini huweza kupata nguvu ya kusoma
Neno la Mungu kwasababu Mungu hutumia Neno kutujibu mahitaji yetu
tuliyo yapeleka kwake.kupitia Neno la Mungu,huweza kutuonya,kutufariji na
kutuelekeza.Faida kubwa tunayo pata ni kwamba Roho Mtakatifu ndiye Anaye
tusaidia kulijua Neno baada ya kumwomba Mungu.1Timotheo 2:1
Ebrania 4:12”Maana Neno la Mungu li hai,tena lina Nguvu, tena lina ukali
kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya
nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyo ndani
yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudu
ya moyo.’’ Shetani huweka vizuizi vikubwa sana kwa
waamini katika swala la kupata muda wa maombi na kusoma Neno.
Pia yapo mahusiano makubwa sana kati ya vitu hivi viwili Maombi na Neno
kwasababu Maombi bila Neno hayana nguvu pia kusoma Neno bila ya kumwomba Mungu
akufundishe hakuna faida pia. Neno ni chakura cha mwamini pasipo
Neno hakuna kukua kwasababu mtu wa ndani hudumaa anapo kosa Neno/chakula na hupelekea
kufa.
(ii) Mahusiano ya karibu na
Mungu hujengwa.Mawasiliano hukuza Mahusiano kwa hiyo kupitia maombi mahusino
makubwa huzaliwa baina ya Mwamini na Mungu .mfano katika hali ya kawaida
kabisa Inajulikana pale ambapo mahusiano ya
watu yanapo kuwa mazuri zaidi ndipo watu hawa huwa karibu sana .lakini pale
ambapo hakuna maweasiliano pia mahusiano huwa mabaya ambapo watu hawa hawawezi
kujuana vizuri kwa undani ukiringanisha na wenye ukaribu.Ndivyo hivyo kwa Mungu
,Mahusiano huwa makubwa sana hata mwamini kutambua siri
nzito kutoka kwa Bwana ni pale tu ambapo mahusiano yanapo kuwa makubwa.Mungu
huachilia siri/maelekezo mengi kwa Yule mwamini Ambaye yuko naye karibu
sana.soma 1samweli 3:10,Daniel 9:21.
(iii) Majukumu ya k i-Mungu huyapokea.
Ipo siri kubwa sana juu ya mawasiliano[maombi] kati ya mwamini na Mungu,
kupitia Maombi Mungu huachilia majukumu yakufanya kwa
mwamini.
mfano ; Samweli , Musa
,Yakobo. Yakobo-kupitia ndoto Mungu aliachilia majukumu mengi kwa
mtumishi wake huyu. Ibrahimu, Mwanzo 22:1-4,
Mungu alimpa majukumu ya kufanya
Ibrahimu pale alipo kuwa na mawasiliano mazuri naye.hata wewe Mtu wa Mungu
tegemea kupewa majukumu mengi zaidi endapo tu utadumisha na kukuza mahusiano na
Mungu. Musa, kutoka 3:4-10.mtumishi
wa Mungu huyu alipo kuwa na mahusiano mazuri na Mungu kupitia Maombi Mungu
alimweshimu na kumpatia majukumu ya kufanya.rejea mstari wa 10;Mungu alimpa
majukumu mtumishi wake Musa baada ya kukubali na kuonesha nia ya
kweli katika upande wa mawasiliano.Note;Mjukumu wakati wote mtu
huweza kupewa kulingana na umri alio nao.hasa katika uwezo wa kiakili.swali
je,anaweza kutunza siri na kumbukumbu vizuri,vivyo hivyo katika Mambo ya
Ki-Mungu,Mungu huachilia majukumu kwa waamini kulingana na kiwango cha kiroho cha mtu
husika.Waefeso 3:20. Kiwango chako cha nguvu za Mungu zilizopo
ndani yako huwa sababisho kwa Mun gu kuachilia mambo makubwa au madogo.Mwanzo
18:16-17.
(iv) Humwezesha Mwamini
kushinda Majaribu.
kupitia mahusiano mazuri na Mungu
kwa njia ya maombi Mungu huweza kumwonekania mwamini kwa namna ya tofauti sana
pasipo hata yeye kujua. Zaburi 50:15.‘‘Ukaniite
siku ya mateso,nitakuokoa, na wewe utanitukuza’’.
Bwana mwenyewe anathibitisha kuwa
kupitia mawasiliano(maombi)utamwita nay eye atakuokoa katika hilo jambo ambalo
utakuwa unapitia.
Ayubu 22:27-30; Utawasiliana na Mungu na yeye atakusikia,kupitia
maombi mipango na ratiba Bwana ataionesha hata
kama changamoto zitakuja lakini Bwana atakuvusha na kukuinua tena katika
kusudi lako.
Zaburi 22:23-24. Bwana anapenda mawasiliano yetu na yeye yawe katika uhusiano
ulio safi kabisa na hakika Mungu lazima Afanye.
MUHIMU: Kama
ilivyo katika maisha ya kawaida watu wawili wanapo kuwa karibu ndipo huanza
kujuana kwa undani sana mfano,mambo ya kufahamu,kimahusiano na kimichezo.
kama hawana mahusiano
usitegemee kujuana kwa undani zaidi but juu juu tu.kiroho lazima
ifike sehemu kama kanisa la kristo tuamke na kumtambua Mungu wetu
kwa namna hii.Mungu anahitaji uhusiano mkubwa na sisi ili aweze kuachilia majukumu
mbalimbali ndani yetu ya kufanya.